samsun
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 7,386
- 5,962
Wakuu nadhani mko poa kama mimi.
Kama kichwa cha habari kinavyosema " Wacha tubaguliwe tu,hakuna namna." Imekuwa ni kawaida kukuta wazungu/waarabu/ wahindi na jamii zingine nyeupe "kuwakashifu" watu wenye rangi nyeusi,hili jambo si zuri na ni lakupigwa vita Duniani kote.
Lakini wakati sisi (weusi) tunataka kuheshimiwa kwa rangi yetu (ni jambo zuri tu wala sio baya tukaheshimiwa) je kweli sisi wenyewe tunaheshimiana kwa tofauti zetu ????
Kwani si ndio sisi tunabaguana wenyewe kwa wenyewe huko kwenye mahotel makubwa hapa nchini mweusi mwenzetu akivaa Sendo haruhusiwi kuingia ndani lakini anakuja mzungu kavaa kipenzi na ana ndala anaingia ????
Kwani si ndio sisi tunamrukisha kichura chura mweusi mwenzetu kwa kukatiza Ikulu,lakini wanakuja wazungu wanapita na hawafanywi kitu na ukiwauliza wanausalama wanakuambia usitufundishe kazi ???
Kwani si ndio sisi wa kabila fulani tunajiona ni bora kuliko hawa wa makabila mengine ??????? ( wanafikia hatua hata hawatakiwi kuolewa/kuoa kutoka nje ya kabila lao na ole wako uoe/uolewe na kabila lisilo lenu utatengwa kama sio kuchukiwa na ndugu zako wewe na mke/mume wako)
Kwani si ndio sisi wa dini fulani ni bora kuliko wale wa dini ile ???? ( mtatukanana,kupigana, na hata muarabu/muisrael/mzungu anakuwa bora kuliko yule mweusi mwenzako, kisa ni wa dini tofauti na yako )
Kwani si ndio sisi wa kaskazini/kusini/magharibi/mashari/ kati ni bora kuliko wale wa kutokea upande ule wa TZ.
Kwani mauaji ya Albino (zeruzeru) yapo nchi gani za weupe au weusi ?????
Mi nadhani niishie hapo kwa leo,kama vipi ongezea rekebisha lakini pia ukijisikia kutukana tukana tu usiogope.