TTCL Je Wametoa SIM Peke yake?

TTCL Je Wametoa SIM Peke yake?

smak786110

Member
Joined
Jan 24, 2008
Posts
90
Reaction score
4
Is it true that TTCL are now selling SIM CARDS only also ?

Nilitaka sana, kama wanatowa...

SMS tariff ni zuri ya TTCL!
 
Is it true that TTCL are now selling SIM CARDS only also ?

Nili taka sana, kama wanatowa...
SMS tariff ni zuri ya TTCL !

...muda mrefu tu wameanza kuuza hizo SIM Cards pekee, tatizo ni kuwa unapoinunua haiwezi kufanya kazi kwenye simu yako ya GSM. Ni lazima uwe na simu yenye mfumo wa CDMA ambazo wanaziuza wao na ma-Agent wa kampuni ya HUAWEI kwa hapa nchini. Kwa hiyo usije ukanunua SIM Card ya TTCL kwa matumaini ya kuiweka kwenye simu yako unayotumia sasa na Card ya GSM inayotumiwa na Zain, Voda na Tigo. Ita-block.
 
naona umefika wakati sasa ttcl watoe na line ambazo zina support mfumo wa gsm. maana mfumo wa cdma kwa hapa tanzania simu zake ni chache sana nyingi ni za gsm.
 
Ni nini manufaa ya kutumia card za TTCL, je zina unafuu wa bei iwapo mtu atakuwa na simu ya CDMA?
 
...muda mrefu tu wameanza kuuza hizo SIM Cards pekee, tatizo ni kuwa unapoinunua haiwezi kufanya kazi kwenye simu yako ya GSM. Ni lazima uwe na simu yenye mfumo wa CDMA ambazo wanaziuza wao na ma-Agent wa kampuni ya HUAWEI kwa hapa nchini. Kwa hiyo usije ukanunua SIM Card ya TTCL kwa matumaini ya kuiweka kwenye simu yako unayotumia sasa na Card ya GSM inayotumiwa na Zain, Voda na Tigo. Ita-block.

Sasa napenda kuuliza kama TTCL wanatumia card za CDMA ni kwa nini au ni kipi cha zaidi nitakachokipata kwa kununua card hizo? Nauliza hivyo ili kutaka kujua operator yupi Tanzania anaweza kunipa huduma zipi na kwa unafuu gani. Natanguliza shukrani.
 
TTCL nadhani walipata tenda "nzuri" kutoka kwa Hauwei ndo maana wakaweka CDMA hawakuangalia market inasemaje.

Unafuu upo Tigo, 1tsh per sec calls. Na SMS 500Tsh unatwanga all day! tena Juzi juzi walifanya 250Tsh!! Personally situmii, ila nasikia service sio mbaya siku hizi.
 
Sasa napenda kuuliza kama TTCL wanatumia card za CDMA ni kwa nini au ni kipi cha zaidi nitakachokipata kwa kununua card hizo? Nauliza hivyo ili kutaka kujua operator yupi Tanzania anaweza kunipa huduma zipi na kwa unafuu gani. Natanguliza shukrani.

...Mmmm, hapa itabidi tusubiri mtaalamu kutoka TTCL kama ni 'mwenyeji' humu atufafanulie. Kidogo ninachofahamu ni kuwa CDMA ni mfumo mpya wa mawasiliano ambao utachukua nafasi ya GSM kama GSM ilivyochukua nafasi ya Analogue. Hata Zantel wanatumia CDMA katika baadhi ya huduma zao.Tusubiri Mtaalamu...
 
CDMA ni teknolojia mpya ya mawasiliano. kitu cha ziada unachoweza kupata kwenye simu hii ni mawasiliano ya internet kama utanunua simu yenye uwezo huo au kununua data card ya kutumia kwenye computer yako.

Alianza TTCL, lakini sasa hivi Zantel anatoa huduma hizi katika miji mingi (namba za 077 50XXXXX. Benson online pia wana CDMA ambayo haiingiliani na TTCL au Zantel. Kampuni mpya inakuja kwa jina la Dovetel na teknolojia hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom