Mjukuu wa kiume wa Waziri Mkuu wa Zimbambwe mheshimiwa Morgan Tsvangirai amefariki baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea nyumbani kwa bwana Tsvangirai juzi jumamosi iliopita.
Mtoto huyo aitwae Shaun ambae alikuwa ana miaka minne, alikuwa ni mtoto wa mtoto wa kiume wa mtoto wa pili wa Mheshimiwa Tsvangirai aitwae Garikai ambae anaishi nchini Canada ambae bado yupo mjini Harare na familia yake kufuatia msiba wa bibi yake Shaun, Susan ambae alifariki mwezi wa March mwaka huu.
Ni juzijuzi tu mheshimiwa Tsvangirai amerudi kazini baada ya maombolezo ya msiba wa mke wake Susan ambae walikaa kwa miaka 30.
Mwenyezi Mungu airehemu roho yake mtoto Shaun, Amen.
Source: Sky news.