Trump Vs Snoop

Na ndo mana nikasema we are far miles away from them,may be miaka mingi ijayo tutakua katika level yao
Hapana, hiyo ingekuwa kweli tu kama tungekuwa tunalenga hatma zinazoshabahiana...bahati mbaya ni kwamba tunakoelekea ni kinyume na wao hivyo kufikia level moja hakuwezekani. Utofauti wetu utazidi kupanuka na hizi grafu haziwezi kukutana mpaka hapo tutakapobadilisha mwelekeo wetu.
 
Sahihi kabisa
 
Ndio maana kwetu rais ukimsema kidogo tu utaambiwa "umetoa kauli za kumuudhi rais" na hakika utafungwa. Labda tusubir tukifika rais wa 30 hivi tutaweza kuwa sawa.
Pia bado tukumbuke kwamba hupaswi kuanza walipoanzia waliokutangulia. Jaribu kuanzia pale walipo au hatua kama moja tu nyuma yao. Vinginevyo turudi zama za mawe màana hapo kati tulishapoteana.

Pia si ajab mkasikia ninatafutwa kwa kuandika raisi badala ya Raisi.
 
Namuona Trump akipewa makavu na TI .

Kweli wenzetu wako mbali sana kwenye uhuru wa kuongea .

Hapa hata ukiita mtu bwege .........

Duuh hii ingishii ya troubleman sijaelewa ata moja. Naona chenga tuu
 
Ngoja kwanza.

Marekani wameanzisha nchi yao 1776, haki ya kusema imeingizwa kama rekebisho la kwanza la katiba, mwaka 1791, miaka 15 tu baada ya uhuru. Kwa hiyo toka mwaka 1791 ulikuwa unaruhusiwa kwenda njia panda hadharani kumchanana chana Rais.

Kwa nini sisi ituchukue miaka 200?

Lakini kingine, sisi tuna blueprint ya kuiga, au desa la kuigilizia kama ni mtihani, wao wamepitia mitihani hii bila mwalimu, bila tuition wala madesa ya kuibia.

Sisi tunatakiwa tuwe tumefika hapo tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…