Trump vs Obama

Umejiuliza uchumi ulikuwaje wakati wote walipochukua madaraka?
Mbona Jiwe alikuta uchumi kipindi cha JK una nafuu akaudidimiza chini zaidi?Trump kupeleka uchumi juu anastahili pongezi!
 
Sasa hapo si unaona Trump kampiga bao obama kona zoote
Mimi nakaa Marekani naelewa hali halisi ilivyo, sasa hivi kuna wasiwasi wa kuja kwa recession kwa kuwa pesa nyingi ziligawiwa kwa matajiri ambao badala ya kuwekeza nchini wao wanaziopeleka nje ya Marekani ili wasilipe kodi.

Huo uchumi mzuri unaouona ni kutokana na sera za Obama ambazo ziliitoa Marekani kwenye recession iliyosababishwa na vita na sera mbovu za taxcut wakati wa Bush. Trump alikuta teyari uchumi umeanza kushika kasi, akaendelea nao ila kutokana na sera zake za tax cut atarudisha nchi kwenye recession tena muda si mrefu.

Hizi sera za Reaganomics (taxcut) za republiCANT zimekuwa zikiharibu uchumi wa Marekani toka kipindi cha Reagan, kila Rais anayefuata sera hizi anapomaliza muda wake nchi inakuwa hoi (Reagan, Bush Sr, Bush Jr, na sasa Trump.)
 
Mbona Jiwe alikuta uchumi kipindi cha JK una nafuu akaudidimiza chini zaidi?Trump kupeleka uchumi juu anastahili pongezi!
Uchumi haukuwa nafuu wakati wa JK, kilichotokea ni kuwa kulikuwa na pesa chafu nyingi mtaani ambazo zilikuwa zikizagaa zagaa, hivyo watu wakadhani uchumi ni mzuri. Uchumi ule wa JK ulikuwa ni uchumi feki usio na msingi wa uzalishaji.
 
Kumbe na wewe umeingizwa mkenge na fake news kama CNN.Mwacheni Trump apige kazi.Hiyo recession ni ndoto za alinacha!
 
Kumbe na wewe umeingizwa mkenge na fake news kama CNN.Mwacheni Trump apige kazi.Hiyo recession ni ndoto za alinacha!
Siangalii CNN nimejionea haya kwa miaka kadhaa.

Nimeshuhudia utawala wa marais toka kipindi cha Clinton-Bush-Obama-Trump ninaelewa fika sera za taxcut zinavyoharibu uchumi.

State yangu ni RepubliCANT, walikuja na sera hizo wakaharibu uchumi vibaya mno mpaka pesa za kuendesha public schools na libraries zikakosekana.

Milingoti ya alama za barabarani zilikuwa ni za chuma, wakazibadlisha kuwa za mbao kwa kuwa state haina pesa za kutosha. Barabara zimekuwa hazifanyiwi ukarabati kwa muda muafaka kwakuwa pesa haipo.
 
Acha kumlinganisha trump na takataka
 
Acha kumlinganisha trump na takataka


Hii ni trend ya kiasi cha magari yaliyonunuliwa kutoka kwenye tovuti ya federal reserve. Ununuzi wa Magari ni kiashiria cha uelekeo wa uchumi Marekani. Utaona jinsi Obama alivyobadilisha uelekeo wa uchumi ambapo Trump anabembea nao.
 
Haina hoja ya maana hata moja .. Kila kitakachowekwa humu utasema ni masalia ya Obama.. Wewe ni wa kupuuzwa tu
 
Haina hoja ya maana hata moja .. Kila kitakachowekwa humu utasema ni masalia ya Obama.. Wewe ni wa kupuuzwa tu
Mimi nimekupa takwimu kutetea hoja yangu na wewe nipe takwimu zako.
 
Heee! Habari za huko baba mkuu! cha moto.

umekaa miaka mingapi ?
 
Kwani mleta mada alichoweka hapo huu sio takwimu ?? Si mmeishia kusema ni atmosphere ya Obama
Wewe wa wapi wewe, ubisha vitu usivyovijua, nimekupa chart kutoka tovuti ya Federal reserve, wao ndiyo wanaohusika na uchumi na mambo yote ya fedha Marekani halafu unaleta porojo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…