Trump vs CNN

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Wadau nini kinachoendelea kati ya shirika la utangazaji CNN na Rais mteule wa Marekani Donald Trump, imefikia hatua Donald Trump katika mazungumzo yake na waandishi wa habari alikataa mwandishi wa habari wa cnn asimuulize swali. Je hii ni dalili kwa taifa kubwa la kidemokrasia linaelekea kuanza kuviminya vyombo vya habari ?
 
Siasa zina mambo mengi sana. Tunachokiona ni kipande kidogo tu.

Ni kwenye siasa tu MTU anaweza kukwambia njano ni nyeusi huku ndani akiwa anajua fika kwamba ni njano, mbaya zaidi njano hiyo hiyo anaweza kukwambia ni kijani kutegemea maslahi au malengo yake.
 
Wadau nini kinachoendelea kati ya shirika la utangazaji CNN na Rais mteule wa Marekani Donald Trump, imefikia hatua Donald Trump katika mazungumzo yake na waandishi wa habari alikataa mwandishi wa habari wa cnn asimuulize swali. Je hii ni dalili kwa taifa kubwa la kidemokrasia linaelekea kuanza kuviminya vyombo vya habari ?

Vyombo vya habari vya wamarekani vina unafiki sana, wakiamua kukuchafua wanakuchafua Dunia nzima, yeye anawajua hao zaidi ya sisi tunavyowajua, mwache a deal nao kadiri ya anavyoona swahihi
 
Mainstream media nyingi za Marekani ikiwemo CNN hawakumuunga mkono Trump wakati wa kampeni.....walikuwa behind Clinton. Waliendesha propaganda nyingi za kumchafua kipindi hicho.

Hata baada ya Trump kushinda uchaguzi bado CNN hawakomi kumchokonoa na hivi majuzi tu CNN walirusha taarifa kuwa Urusi wana siri nyingi za mienendo miovu ya Trump na itabaki kuwa siri kubwa ya Urusi. Eti hiyo 'leak' wameipata kutoka shirika la Ujasusi la Uingereza.

Kilichomkera Trump ni kiherehere cha CNN kurusha taarifa ambazo usahihi wake haujathibitishwa kwa asilimia 100 kitu ambacho ni kinyume na maadili ya uandishi wa habari. Ikumbukwe kuwa baadhi ya TV za Marekani ziligoma kurusha taarifa hiyo kwasababu hazikua na uhakika wa usahihi wake.

Kwangu mimi, Trump alikuwa sahihi coz it seams CNN wana agenda ya siri dhidi ya Trump.
 
Hahaa not you not I won't give you a question. ..huyu dingi akimaliza salama sijui?yasije kuwa ya Reagan
 
Back
Top Bottom