Trump hatanii, afuta misaada ya kiusalama Pakistan

Trump hatanii, afuta misaada ya kiusalama Pakistan

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Misaada ya kiusalama kwa Pakistan yenye thamani ya takriban dola milioni 900 itasitishwa hadi pale Pakistan itakapochukua hatua madhubuti kupambana dhidi ya kundi la wanamgambo wa Afghanistan la Taliban na la Haqqani

Hatua hiyo iliyotangazwa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema inaonyesha kukerwa kwa utawala wa Rais Donald Trump kuwa Pakistan haijachukua hatua za kutosha dhidi ya makundi hayo mawili ambayo yamekuwa yakiitumia nchi hiyo kama sehemu ya kujificha na kufanya mashambulizi katika nchi jirani ya Afghanistan na kuwaua wanajeshi wa Marekani, wa Afghanistan na wa kutoka nchi nyingine.

Ufadhili huo utakaositishwa utaathiri ununuzi wa vifaa vya kijeshi, mafunzo, huduma nyingine za kijeshi na mpango wa kupambana na ugaidi. Akiwahutubia wanahabari, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert amesema hatua hiyo ya kusitisha ufadhili, haitaathiri misaada inayotolewa kwa raia wala zile za kusaidiai uchumi wa Pakistan

Miradi ya kijeshi itaathirika

Nauert amesema fedha hizo huenda zikadihinishwa kutolewa iwapo Pakistan itachukua hatua zinazostahili kukabiliana na makundi ya kigaidi, wakiongeza wanatumai Pakistan itaona hatua hiyo kama kupewa afueni na sio kupewa adhabu. Bunge la Marekani limefahamishwa kuhusu uamuzi huo wa kuistishia Pakistan misaada.

Pakistan kwa muda mrefu imekanusha shutuma kuwa imeshindwa kupambanana na makundi ya wanamgambo yanayopambana dhidii ya majeshi ya Afghanistan na ya kigeni kutokea upande wa pili wa mpaka.

Uhusiano kati ya Pakistan na Marekani umekuwa tete tangu tarehe mosi mwezi huu wakati Rais Donald Trump alipoishutumu nchi hiyo kupitia ukurasa wa Twitter kuwa licha ya kupewa misaada ya takriban dola bilioni 33, katika kipindi cha miaka 15 iliyopita inafanya kile alichokitaja danganya toto kwa kujifanya kupambana na ugaidi na wakati huo huo, kuwaruhusu wanamgambo wa Taliban na Haqqani wanaosakwa na Marekani kuitumia nchi hiyo kama ngome yake na hivyo kuwafanya viongozi wa Marekani kuonekana wapumbavu.

Pakistan imezitaja shutuma hizo za Trump kama zisizoelewa kabisa na zinazokinzana na kauli za waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson na wa ulinzii James Mattis waliofanya ziara hivi karibunu Islamabad kwa kile kinachotajwa kujenga uaminifu kati ya Marekani na Palestina.

Pakistan imeishutumu Marekani kwa kuitumia kama kisingizio kwa kushindwa kuleta amani nchini Afghanistan. Siku ya Alhamisi wiki hii, wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia iliishutumu Pakistan kwa ukiukaji mkubwa wa uhuru wa kidini na kutangaza inaiweka nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazofuatiliwa kwa undani.

Chanzo: DW
 
Kwani Osama walimuuza bei gani?..wapambane na hali zao!..
 
Na Tanzania walisha sitisha kuangiza cement kutoka pakistan, kama wanasupport ugaidi wacha wale jeuri yao
 
Trump hapo kakurupuka...

Kila mmoja anafahamu jinsi Pakistan ilivyo muhimili muhimu kwa Marekani kwenye sera zake the so called vita dhidi ya ugaidi.

Nasema "the so called vita dhidi ya ugaidi" kwa sababu ni Wamarekani wenyewe, kwa kushirikiana na Pakistan ndio waliwatengeneza Mujahideen kutokea Pakistan na kuwaingiza Afghanistan ili wakapambane na Urusi... kwahiyo wanavuna walichopanda!!!

Wakati CIA wanatumia Pakistan's Inter-Services Intelligence kuwaunda Mujahedeen, walikuwa wanatumia makundi ya kidini waliodhani hawakuwa na malengo... and YES, hawakuwa na malengo manake mara baada ya kuwafurumusha Warusi, wakaanza kutwangana wenyewe kwa wenyewe kugombea madaraka!!

Kilichofuata hapo ni kuzaliwa kwa Taliban chini ya Mullar Omar.

Matokeo yake, hadi leo Pakistan's Inter-Services Intelligence ndani yake ina watu wenye itikadi za kidini ambao wapo tayari ku-betray government operations na kuwatumikia magaidi!

So, to cut loose Pakistan, ni kuwapa ushindi hawa intelligence officials wanaowatumikia Taliban na matokeo yake hali ya Marekani huko Afghanistan itakuwa mbaya maradufu na salama yao itakuwa ni kufangasha virago na kuondoka!

But all in all, binafsi sijawahi kuwa na shida sana na Taliban... hawa jamaa ni kama Hezbollah!!

Taliban hawana shida na mtu wala taifa lolote; at least as for now. Taliban ni na Afghanistan yao, and of course, na Pakistan yao ambao na wenyewe wanavuna walichopanda!!! Sijawahi

Na kabla ya September 11 iliyopelekea Marekani kuwashambulia Taliban, sikuwahi kusikia Taliban wakiendesha mashambulizi kwa taifa lolote nje ya Afghanistan... na in fact, hadi sasa sijawahi kusikia isipokuwa ni kwa Afghanistan yenyewe na Pakistan!
 
Back
Top Bottom