Trump aongeza ushuru kwa bidhaa za China

Trump aongeza ushuru kwa bidhaa za China

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Rais Donald Trump wa Marekani, ameagiza kuongezwa kwa ushuru kwa karibu bidhaa zote za China zilizosalia na zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 300.

Trump ametoa uamuzi huo hapo jana Ijumaa kupitia ukurasa wake wa Tweeter, huku hatua yake hiyo ikizidi kongeza mvutano wa kibiashara baina ya Marekani na China inayoshikilia nafasi ya pili kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani.

Kauli ya Trump, imetolewa kabla ya saa 24 kupita tangu Marekani iamue kuongeza ushuru kwa bidhaa za Kichina zenye thamani ya dola bilioni 200, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya hapo awali.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya Rais Trump kuituhumu China kukwepa majukumu yake. Kutokana na hatua hiyo, China imesema mazungumzo yataendelea ili kutafuta suluhisho la mgogoro huo
 
Trump kaona China ndio supporter number moja Wa taifa korofi LA north korea.go go trump
 
Binafsi, bado Political Economy ya mataifa haya makubwa inanipiga chenga sana. Ninafahamu Marekani ina uchumi mkubwa, lakini ninashindwa kuelewa uchumi wake hutegemea nini kama tunavyoona sasa hivi kila taifa analinyoosha. Ni mwendo wa vikwazo tu, je, yeye haathiriki kwa vikwazo anavyoweka mwenyewe? Kwa mfano, yeye hauzi China?

Katika hili la China, ni wazi China amekuwa mpole pamoja na ujeuri wake. Na Marekani wala haoneshi kusita.
 
Binafsi, bado Political science ya mataifa haya makubwa inanipiga chenga sana. Ninafahamu Marekani ina uchumi mkubwa, lakini ninashindwa kuelewa uchumi wake hutegemea nini kama tunavyoona sasa hivi kila taifa analinyoosha. Ni mwendo wa vikwazo tu, je, yeye haathiriki kwa vikwazo anavyoweka mwenyewe? Kwa mfano, yeye hauzi China?

Katika hili la China, ni wazi China amekuwa mpole pamoja na ujeuri wake. Na Marekani wala haoneshi kusita.
Katika Ile trade balance China anakwenda kuumia zaidi kwasababu China ndio anaeuza bidhaa nyingi Kwa Marekani.
 
Angalia hizo chart mbili ya Marekani na Mchina. Ni Nani atakayeumia. Hata hivyo China alishafungiaga baadhi ya makampuni ya Marekani kuoperate nchini china mfano Facebook, WhatsApp, Google, Amazon,
OK. Kwahiyo Mchina hawezi kumkomesha US hata kwa hicho kidogo cha US?
Marekani ataumia but China anakwenda kuumia zaidi. Kwasababu China ndio anayoitegemea Marekani kuexport zaidi bidhaa. Ujue Marekani ina washirika wenye nguvu kiuchumi ambao baadhi ni adui wa China mfano Japan, bara la Ulaya, na India . Lakini hii itakuwa nafasi Kwa nchi zingine zinazochipukia kiviwanda kuuza bidhaa zake Marekani
Screenshot_20190511-201340.jpeg
Screenshot_20190511-201256.jpeg
 
Huyu bwana ana kiburi sana manake soko lake la ndani linamtosha, haujasikia akisema juzi kwamba sio lazima tufanye biashara na china, tunaweza fanya business wenyewe hapa
Binafsi, bado Political Economy ya mataifa haya makubwa inanipiga chenga sana. Ninafahamu Marekani ina uchumi mkubwa, lakini ninashindwa kuelewa uchumi wake hutegemea nini kama tunavyoona sasa hivi kila taifa analinyoosha. Ni mwendo wa vikwazo tu, je, yeye haathiriki kwa vikwazo anavyoweka mwenyewe? Kwa mfano, yeye hauzi China?

Katika hili la China, ni wazi China amekuwa mpole pamoja na ujeuri wake. Na Marekani wala haoneshi kusita.
 
Mbona kila siku KELELE si aeke hivyo vikwazo mbona baadae huwa anarudi na kutaka mazungumzo?? KESHO KUTWA UTASKIA TRUMP AKARIBISHA MAZUNGUMZO NA CHINA
 
Binafsi, bado Political Economy ya mataifa haya makubwa inanipiga chenga sana. Ninafahamu Marekani ina uchumi mkubwa, lakini ninashindwa kuelewa uchumi wake hutegemea nini kama tunavyoona sasa hivi kila taifa analinyoosha. Ni mwendo wa vikwazo tu, je, yeye haathiriki kwa vikwazo anavyoweka mwenyewe? Kwa mfano, yeye hauzi China?

Katika hili la China, ni wazi China amekuwa mpole pamoja na ujeuri wake. Na Marekani wala haoneshi kusita.
china hununua karibu nusu ya ndege za boeng za marekani.hiyo ni moja tu.
 
Alafu utasikia mtu anatoka chanika anakwambia marekani hana nguvu kwa sasa duniani.... [emoji23][emoji23]
Wasamehe mkuu, ni uelewa mdogo wa mambo ya uchumi wa Dunia.

Kwa sasa marekani kiuchumi ana upperhand dhidi ya china. Malalamiko ya Marekani yana mashiko sana.

China aliporuhusu biashara binasfi na uwekezaji makampuni mengi yaliyoenda ni kutoka Marekani. Makampuni hayo yakarubuni serikali za marekani yapunguziwe ushuru kuingiza vitu vyao Marekani, yaani kitu kikitoka China kipigwe ushuru wa chini lakini kitu hicho hicho kikitoka Marekani kwenda China kipigwe bei kubwa, mfano gari moja toka China kwenda USA ushuru 2.5% lakini gari hilo hilo kutoka Marekani kwenda China 25%, ikapelekea bidhaa za kichina kuuzwa sana USA kuliko hata bidhaa za ndani za Marekani. Na China ilikua inalobby tawala zilizopita ili waendelee kufaidi.

Kwenye kampeni Trump aliahidi kuishughulikia China, nakumbuka hata serikali ya China ilitoa tahadhari ya matamshi ya Trump wakati wa uchaguzi wakawasihi Wamarekani kua makini ili wasije kuharibu ubhsiano wao wa muda mrefu(wakiwa wanamzungumzia Trump iwapo atashinda ataharibu uhusiano kibiashara, hivyo walikua wanamhofia toka awali na hawakutaka ashinde, walijua atakuna kuwaharibia).

Trump pia anasema China imekua ikikiuka mikataba ya kibiashars ya kimataifa kwa kulazimisha kila kampuni inayotaka kuwekeza huko itafte mbia da ndani kwa lazima, yani lazima kuwe kampuni ya nje iwe na partner wa kichina vinginevyo haitaruhusiwa, hivyo kupelekea makampuni ya kichina kuiba teknolojia ya Marekani kwa nguvu, forceful transfer of technology.

Kwa hapa China kazi anayo. Trump atawanyoosha.
 
Mmarekani atabaki kuwa mbabe
Yoyote anaefurukuta anaishia kula vikwazo, sio Urusi sio China sio Ulaya, Afrika ndio kabisa sisi ni kama michepuko, unajua mchepuko unavyonywea kwa sponsor. Marekani anamuwekea vikwazo urusi vya kifedha, juzi urusi imesema itabidi watengeneze internet yao mana Marekani akija kuwawekea vikwazo na akawazimia internet watahangaika.. hilo wazo pia Marekani ataliwekea vikwazo sio siku nyingi washindwe kulitekeleza.
 
Yoyote anaefurukuta anaishia kula vikwazo, sio Urusi sio China sio Ulaya, Afrika ndio kabisa sisi ni kama michepuko, unajua mchepuko unavyonywea kwa sponsor.
😂😂😂😂 ila ukitukuta kwenye vijiwe vyetu tunapiga soga, haukawii kusikia "North korea aka kiduku ana bomu ilo linaangamiza marekani nzima" ukifungulia media za kimataifa utasikia "marekani imeshikilia meli ya norh korea" yaani vurugu tupu.
 
Mchina anampelekesha sana USA
Jamaa hawana utani likija suala la kutengeneza hela na itakapofika mwaka 2020 watu 780m watakuwa na middle-class income
Kampuni ya Starbucks ya USA ilifungua baishara ya coffee miaka 20 iliyopita na mpaka sasa wameweza kuwa na sehemu 3000
Miaka 2 iliyopita China wakaona isiwe shida nao wakaanzisha kampuni yao ya kuuza kahawa inayoitwa luckin coffee huwezi amini walikuwa wanafungua sehemu moja kila masaa 4 na walianza na 9 na kuongezeka mpaka 2073 kwa miaka 2 tu
Hapo ndio nasema wako very aggressive likija suala la biashara.

Tuache ushabiki wa kimarekani ila jamaa hawa hawana utani
Trump anajua anawahitaji sana kwa bidhaa zao kwani ziko chini sana kutokana na cheap labour ukifananisha na mishahara yao
 
... haya ndio madili ya Bw. Trump; kuyashikisha adabu mataifa vichwa maji. Sie tubaki kwenda kuzindua sijui msimu wa maharage; aaaaah!
 
Mchina anampelekesha sana USA
Jamaa hawana utani likija suala la kutengeneza hela na itakapofika mwaka 2020 watu 780m watakuwa na middle-class income
Kampuni ya Starbucks ya USA ilifungua baishara ya coffee miaka 20 iliyopita na mpaka sasa wameweza kuwa na sehemu 3000
Miaka 2 iliyopita China wakaona isiwe shida nao wakaanzisha kampuni yao ya kuuza kahawa inayoitwa luckin coffee huwezi amini walikuwa wanafungua sehemu moja kila masaa 4 na walianza na 9 na kuongezeka mpaka 2073 kwa miaka 2 tu
Hapo ndio nasema wako very aggressive likija suala la biashara.

Tuache ushabiki wa kimarekani ila jamaa hawa hawana utani
Trump anajua anawahitaji sana kwa bidhaa zao kwani ziko chini sana kutokana na cheap labour ukifananisha na mishahara yao
Nadhani kuna mahala uelewa wako unapungukiwa na vitu. Tafta vyanzo sahihi vya taarifa zako, achana na hadithi za kwenye kahawa na kashata.
 
Back
Top Bottom