Trump Ahofia Kung'olewa Kabla Muhula Wake Haujaisha.

Juuchini

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
1,923
Reaction score
2,735
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo kali kwa wabunge wa chama chake cha Republican, akidai kuwa wasiposhinda uchaguzi wa katikati ya muhula wa Novemba 2026, wapinzani wake wa chama cha Democratic watamng'oa madarakani kwa kumfungulia mashtaka ya kikatiba.

Akizungumza Jumanne katika mkutano wa ndani wa wabunge hao mjini Washington, Trump alisisitiza umuhimu wa ushindi huo ili kulinda ajenda zake na kuepuka uchunguzi wa bunge.

"Lazima mshinde uchaguzi wa katikati ya muhula, kwa sababu msiposhinda, watatafuta sababu yoyote ya kuniondoa madarakani. Nitang'olewa," Trump amewaambia wabunge hao kwa uwazi.

Katika hotuba yake iliyodumu kwa dakika 84, Trump amewataka washirika wake kuweka kando tofauti zao na kujikita katika kuuza sera za chama kuhusu masuala ya jinsia, huduma za afya, na uadilifu wa uchaguzi, hasa kwa wapiga kura wenye hasira juu ya kupanda kwa gharama za maisha. Amekiri kuwa kihistoria, rais aliyeko madarakani huwa anapoteza viti vingi katika uchaguzi huo, akishangazwa na mwelekeo huo wa fikra za umma.

Huku akijivunia operesheni ya kijeshi dhidi ya kiongozi wa Venezuela, Nicolas Maduro, Trump amekuwa akishinikizwa kuelekeza nguvu zake kwenye masuala ya ndani kama mfumuko wa bei. Hata hivyo, amedai kuwa alirithi tatizo hilo kutoka kwa Democrats na kuwataka Republicans kujivunia kupaa kwa masoko ya hisa.

Trump, ambaye amewahi kufunguliwa mashtaka ya kikatiba mara mbili katika muhula wake wa kwanza (2017-2021) na kuachiwa huru na Baraza la Seneti, kwa sasa anakabiliwa na tishio jipya huku baadhi ya wabunge wa Democratic wakishaanza kuandaa hati za mashtaka dhidi yake kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka katika muhula wake wa pili.
 
Moderator ipelekwe international forum
 
Marekani akitoka Trump hata nchi haipendezi kama super power nation!, tumeshazoea mikwala yake kama kipindi cha Magufuli huku kwetu Tz!, wakati huo ndo mda nilikuwa sikosi hata kuangalia taarifa ya habari kila siku.
 
Marekani akitoka Trump hata nchi haipendezi kama super power nation!, tumeshazoea mikwala yake kama kipindi cha Magufuli huku kwetu Tz!, wakati huo ndo mda nilikuwa sikosi hata kuangalia taarifa ya habari kila siku.
Wenzetu wale hawapendi mikwara ila kufuata katiba na sheria zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…