True Story Of My Life!

Hasa relatives wa kijijini ndio balaa!Nkienda zangu Rombo nikiwa na elf thelathini kwenye mfuko wa suruwali utasikia:"Mjomba, hebu nifanyie kama elf hamsini hivi banda la ng'ombe limebomoka nataka kulikarabati." Ole wako useme huna hiyo elf hamsini utasikia wakilalamika:" Hayo mahela yote mnayopata huko mjini mnapelekaga wapi?

Maskini ya rabbi, ni kweli naishi mjini ila vibiashara vyangu havinilipi zaidi ya laki mbili kwa mwezi.

Jamaa na ndugu waishio kijijini wanafikiri watu wa mjini wana pato kubwa sana.
 

Hiii kweli mkuu, inakera sana hiyo tabia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…