Biashara ya malori kwa sasa transit goods zinalipa sana especially kuelekea Congo (Lubumbashi),Zambia,Rwanda,Burundi na Malawi.
Unahitajika kujenga uhusiano mzuri na clearing agents, unaweza kupata contacts zao kutoka kwenye website ya TRA. Fanya mawasiliano nao either by visiting them and make your company known to them.
Fanya research ya kutosha kuhusu yafuatayo
.Bei za kusafirishia mizigo kwenda destination mbalimbali
.Bai na suppliers wa inputs kama matairi na vipuri
.Madereva wazuri na waaminifu na uwalipe vizuri
.Gari gani zinahitajika sana,box body au za kubeba container?
.Angalia washindani wako wakubwa katika biashara na athari zao kwa biashara yako.
.Mafundi ambao ni full time kwa ajili ya magari yako
Faida ya biashara hii ni kubwa lakini inahitaji involvement ya hali ya juu. Unatakiwa ufuatilie kila details kwa sababu unaweza ukajikuta unawafanyia biashara madereva wako,especially mafuta wanauza sana njiani.
Ikiwezekana safiri na magari yako angalau kila route mara moja ili ujue ni kiasi hali halisi ya barabarani kwa sababu umesema hujawahi kuwa katika biashara hii.
KILA LAHERI MKUU