Trilioni 2.3/- zahitajika reli Mchuchuma hadi Mtwara

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SERIKALI imesema Sh trilioni 2.250 zitatumika kujenga reli ya Mchuchuma, Liganga hadi Mtawara.
Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba alisema gharama hizo zimetokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) mwaka 2006.

Alisema ujenzi wa reli hiyo utategemea utekelezaji wa miradi ya Mchuchuma na Liganga ambayo ni mihimili ya ukanda wa maendeleo ya Mtwara.

"Hivi sasa NDC lenye jukumu ya kutekeleza miradi hiyo liko kwenye hatua ya majadiliano na mwekezaji wa kampuni ya ‘Sichuan Hongda Corporation ambayo ilishinda zabuni mwezi Juni, 2011.

"Majadiliano yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni 2011 pamoja na kusainiwa mkataba wa ubia ili kutekeleza miradi hiyo kwa pamoja, hivyo maandalizi ya ujenzi wa reli katika ukanda wa maendeleo wa Mtwara unategemewa kuanza mara baada ya kuanza ujenzi wa miradi ya Mchuchuma na Liganga, yaani Januari 2012," alisema.

Mfutakamba alisema serikali inatambua umuhimu wa reli hiyo na inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inajengwa kwa wakati.

Mfutakamba alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Mariam Kasembe (CCM) aliyetaka kujua maandalizi ya ujenzi wa reli ya ukanda wa Mtawara: Mchuchuma – Liganga hadi Mtwara yamefikia
hatua gani na yatagharimu fedha kiasi gani.

 
Hizi ndio sehemu za kuwekeza fedha au hata kukopea sio kukopa fedha za wafadhili kulipa mishahara ya wabunge wanaolala Dodoma
 
Back
Top Bottom