Trigger Happy Tanzanian Police, Where are we heading? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trigger Happy Tanzanian Police, Where are we heading?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiwi, Dec 18, 2011.

 1. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  [h=2][/h]

  [h=2]Gari lapigwa risasi saba na polisi[/h]  Dereva wa gari aina ya Toyota Town Hiace amenusurika kifo baada ya gari lake kupigwa risasi saba ubavuni na kutokea upande wa pili kufuatia ubishi uliozuka baina yake na askari polisi alipotakiwa kupeleka gari lake kituo cha polisi kukaguliwa.  Akisimulia tukio hilo jana, dereva huyo, Robert Merengo (31), katika kituo cha polisi cha wilaya, alisema tukio hilo lilitokea saa 3 asubuhi nje ya duka la kuuzia mbao la Maswi Mkohi, ambapo askari wawili waliokuwa na bunduki walipofika sehemu alipokuwa ameegesha gari.


  Alidai kuwa polisi hao walimwamuru ageuze gari na kulipeleka kituo cha polisi na alipowauliza ana kosa gani ndipo walimwambia atoke ndani ya gari huku wakimwelekezea bunduki shingoni.


  Alidai kuwa "nilipoteremka chini walitaka kunipiga ndipo mama mwenye duka, Lucy Maswi alipoingilia kati na kuwauliza kama mnaona gari lina kosa simchukue namba za gari kwani gari hili si la hapa mjini na tajili wake mnamfahamu?
  Kabla mama huyo hajamaliza kuwaeleza walifyatua risasi saba kuingia ndani ya gari mlango wa kushoto na kusababisha watu wa mtaa huo kukimbia ovyo kutokana na mlio huo wa risasi hizo zilizotoboa matundu katika gari hiyo."


  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime, Rorya SSP Sebastian Zakaria alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea kwa tukio hilo ingawa alisema hakuna majeruhi na kudai kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kutoa taarifa baadaye kinachoendelea.


  Hadi tunakwenda mitamboni kulikuwa hakuna taarifa zaidi mbali na gari hilo kubaki hapo kituoni likiwa na matundu ya risasi.
  Wakazi wa mji wa Tarime na vitongoji vyake wamelaani kitendo hicho cha askari kutumia risasi za moto na kuleta mtafaruku katika mitaa hali ambayo wamedai ufyatuaji risasi ovyo ama nguvu zaidi katika ukamataji wa wahalifu wa makosa ya usalama barabarani kwa kutumia bunduki unakiuka haki za watumiaji wa vyombo vya moto.


  Naye mmiliki wa gari hiyo, Boniface Mohere, alisema gari lake lina vibali vyote anasikitika kwa askari kumharibia gari na kutaka kuua dereva kutokana na ubishi wao wenyewe.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


   
Loading...