Wakati sisi tukiwa hapa View attachment 92168 wenzetu wako hapa View attachment 92169
Hivi tatizo ni umasikini au ni matatizo yetu ya kufikiri? Maana hii sio tu huduma, bali ni biashara, tena biashara yenye manufaa kwa taifa na raia. Mfano, kwa basi sasa kutoka Dar kwenda Dom ni masaa 7 hadi nane, wakati Dar - Arusha ni masaa nane hadi tisa. Kwa usafiri wa treni za kisasa Dar - Dom ingechukua 2hrs na Dar - Arusha ingechukua 2.5hrs.
Mimi nafkiri inawezekana, tuache EXCUSE ya umasikini, tufikiri sawasawa, umasikini tunautengeneza wenyewe sasa.
Wakati sisi tukiwa hapa wenzetu wako hapa View attachment 92169
Hivi tatizo ni umasikini au ni matatizo yetu ya kufikiri? .
nimependa mawazo yako
naishi mji ambao una urefu sawa na kutoka dar hadi Arusha yaanizaidi ya km 600
kutoka mji nilipo hadi ilipo familia ni 8 hrs kwa mabasi yao ya kisasa
na tren la umeme ni 6 hrs, hii ni kwa sababu wana single line ya reli na ni nchi tajiri sana
ila kijiografia ina milima.
kujenga double line from Arusha to dar au from dar to Dodoma sio rahisi kwa uchumi wetu
Pili hatuna umeme wa uhakika wa kuwezesha kujengwa kwa line ya umeme usiokatika kwa Tanzania
cha msingi tuwe kwanza na umeme wa uhakika,tusubiri mradi wa Rufiji na Mbeya makaa ya mawe
na ule wa Singida wa umeme wa upeo.
Pili tupate mkandarasi wa kujenga new railyway line walau single line kwa route hizo hadi Kigoma.walau kutoka
Kigoma gadi dar iwe 8 hrs na kutoka Dom hadi dar iwe 3hrs na Arusha hadi dar walau 5hrs
hatuhitaji tren za kasi sana walau zile zinazokimbia 120km/hr inatosha..
Hii itawezekana tukiwa na rais dikteta na awe mzalendo asieogopa watu.
tren kama hizi zinatosha
yale mengine ya kasi zaidi baadae nchi chache wanazo kama german na china, japan..
uko sahihi kabisa....ila niongezee tu....sio lazima treni za umeme....kuna za DIESEL ENGINE zinakimbia hadi 250km/h na za kisasa kabisa.....so hii nadharia kuwa hatuwezi kuwa na treni za kisasa kisa umeme tuifute.....
Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them. Sikushangai, nakuonea tu hurumaHizo picha tu, unajuaje injini ya hiyo treni yetu na hizo za shoga zako huko mamtoni, achilia mbali zaweza kuwa fotoshop?
TAZARA oyeeeee....
Mimi kwanza nafurahi kuona kwamba unaona uwezekano wake. Nimefuatilia jambo hili kwa kina. Sababu ya umeme ndiyo ambayo hata viongozi wa siasa wanaing'ang'ania sana, lakini umeme sio tatizo hata kidogo. Walichokifanya wachina kwa mfano, wametengeneza vyanzo vya umeme specifically kwa miundombinu ya reli - high speed train - umeme ambao hauingii kwenye gridi ya taifa. Hivyo hata umeme ukatike nchi nzima, katika njia za reli upo. Wajapani na wenyewe wamefanya hivyo katika baadhi ya maeneo. Sasa kwa mfano hapa kwetu, ule mradi wa Malagalasi ukawa mahsusi kwa Kigoma na Reli ya kati, ule wa makaa ya mawe wa Mchuchuma ukawa maalumu kwa Reli mpya ya Mtwara - Mamtumbo, Mtwara - Dar, pamoja na Tazara, Pangani kuna mitambo miwili, ule wa pangani na ule wa Hale, hivyo ule mdogo wa Hale ukawa special kwa reli ya Tanga - Arusha, ni jambo linalowezekana kabisa, ni uvivu tu wa kufikiri. Usafirishaji ni biashara inayolipa sana siku hizi, kwa hiyo huo ni uwekezaji sio huduma. Shirika la Reli la Japan linachangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 17, hapo bado maswala mtambuka yanayohusiana nalo.My friend, nchi yetu sio masikini, hivyo ni tatizo la uongozi. Singapore ilipiga hatua za kiuchumi kwa kuwa na viongozi na wananchi waliokuwa na uzalendo na nchi yao. Sasa ukiwa na viongozi ambao kila project ya umeme ni nafasi kwao ya kujitajirisha utaenda wapi? Viongozi wanaohusika na ujangiri, viongozi wanaotetea viongozi wenzao mafisadi na wezi ndio wataleta train za namna hii?
Treni hizi za kasi zinawezekana, lakini si katika mazingira ya umeme usiotosha hata kwa matumizi ya nyumbani tu. Hizi treni zinahitaji umemem wa hakika usio katikakatika au kutegemea mvua, la sivyo utalaza watu njiani kila siku.
Kuna wakati nilimshauri JK kuangalia uwezekano huu kwa reli ya Tazara, kwa kuingia ubia na wachina, kutia ndani na kuipeka hadi Malawi. Reli ya Tazara inawezekana kabisa kuirekebisha na kuweka treni za kasi. Kinachotakiwa ni kuondoa kona zote kali na pia kujenga flyovers kwa kuwa njia za treni za kasi hazihitaji kuwe na sehemu watu, daladala, mbuzi na mikokoteni vinakatisha reli.
Ukiwa na train za kasi reli ya Tazara utafanya Zambia na Malawi wavutiwe pia na bandari ya Dar, kwa maana watapata mizigo yao kwa kasi sana. Na pia abiria wataacha hata kutumia mabasi, ukizingatia safari ya Dar-Mbeya itachukua kama masaa manne hivi. Ila itabidi ujenge seti ya pili ya reli, yaani njia ya kwenda na njia ya kurudi la sivyo treni zitagongana kila siku.
Tatizo Tanzania tunaangalia gharama badala ya faida na pay back period. Tukiingia ubia na Wachina hii project nina uhakika itafanikiwa.
Sasa wakati wengine tunamshauri JK juu ya miradi kama hii, yeye anafikiria ambulance za Bajaji. Huo ndio upeo wake wa miradi ya maendeleo kwa Tanzania.
nimependa mawazo yako
naishi mji ambao una urefu sawa na kutoka dar hadi Arusha yaanizaidi ya km 600
kutoka mji nilipo hadi ilipo familia ni 8 hrs kwa mabasi yao ya kisasa
na tren la umeme ni 6 hrs, hii ni kwa sababu wana single line ya reli na ni nchi tajiri sana
ila kijiografia ina milima.
kujenga double line from Arusha to dar au from dar to Dodoma sio rahisi kwa uchumi wetu
Pili hatuna umeme wa uhakika wa kuwezesha kujengwa kwa line ya umeme usiokatika kwa Tanzania
cha msingi tuwe kwanza na umeme wa uhakika,tusubiri mradi wa Rufiji na Mbeya makaa ya mawe
na ule wa Singida wa umeme wa upeo.
Pili tupate mkandarasi wa kujenga new railyway line walau single line kwa route hizo hadi Kigoma.walau kutoka
Kigoma gadi dar iwe 8 hrs na kutoka Dom hadi dar iwe 3hrs na Arusha hadi dar walau 5hrs
hatuhitaji tren za kasi sana walau zile zinazokimbia 120km/hr inatosha..
Hii itawezekana tukiwa na rais dikteta na awe mzalendo asieogopa watu.
tren kama hizi zinatosha
yale mengine ya kasi zaidi baadae nchi chache wanazo kama german na china, japan..
uko sahihi kabisa....ila niongezee tu....sio lazima treni za umeme....kuna za DIESEL ENGINE zinakimbia hadi 250km/h na za kisasa kabisa.....so hii nadharia kuwa hatuwezi kuwa na treni za kisasa kisa umeme tuifute.....
Swala la kujenga reli mpya halipingiki kwani reli yetu geji yake ni ndogo, kidogo reli ya tazara ni nzima. Lakini pia tunahitaji line mbili katika reli, na hilo linawezekana kabisa. India wanatengeneza vyuma vya reli sasa, na ni dunia ya tatu, hivyo tunaweza kununua kwao. Wao tayari wana treni za kasi ingawa si nchi nzima. Mfano kutoka Bangalore kwenda New Delhi kuna treni za kasi.nashukuru kwa mawazo mbadala
hizo tren bila shaka lazima zijengwe line mpya ya reli kwani haziwezi kumatch na hii tulio nayo kwa sasa.
wazo la kuwa na tren ya umeme wa maji na hii ya diesel nadhani yote mawazo mazuri
kwa vile watendaji wengi serikalini na wanasiasa wanadiawa kumiliki magari ya mizigo na mabasi hawatapenda hii idea