Travelling in Kenyan car through Serengeti

Yaani nilisoma huo uzi na mara moja hisia hizi zilinipita kichwani:
1. Hivi kusafiri toka eneo moja hadi lingine shida tupu. Miundo msingi havimo, licha ya kuwa eneo husika ni wa umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi. Majanga.
2. Katika karne ya 21, bado kuna baadhi ya mataifa yanoyojivunia kutenga na kudhulumu baadhi ya majirani zao.Karne yenye wadadisi wa historia wanasisitiza utakuwa wa kwanza kuunganisha binadamu, hasa tukizingatia umwagikaji wa damu tuliyo shuhudia kwa karne uliopita na wakutisha mno. Kinyume na mwenendo ya uhusiano baina ya binadam binafsi na mataifa, kuna watu binafsi na mataifa ambayo yanaona vyema kuchochea. Niwakumbushe warusi na wamarekani wanashirikiana kwa nyanja mbali ya sayansi na uhandisi kuboresha maisha ya watu wao na umma ya binadamu kwa ujumla. Lipo hata na barabara ya kilomita za kishenzi wanataka kujenga,Halafu unashtukia ripoti kama hizi.
3. Mpaka lini vikwazo ndogo ndogo na vya kuudhi zitazuia biashara iinuke katika hili kanda, zinaitwa "non tariff barriers" na "endless bureaucracy" kwa lugha yazungu.
4.Hivi watz, hili ni jambo la kujivunia au aibu??
 
Quickly hii ni habari ya 2010! It is this ban that led to Madam Kandie to bar tour vans from Tanzania from accessing JKIA and as a result we cut down KQ frequency to JNIA..
 
Kumbe kutoka Arusha mpaka Singida hakuna lami? Hope kikwete alifanya jambo hapo kwani hii ni miji yenye umuhimu sana Tanzania
 
Kumbe kutoka Arusha mpaka Singida hakuna lami? Hope kikwete alifanya jambo hapo kwani hii ni miji yenye umuhimu sana Tanzania

Arusha to Singida road
25112012738%5B1%5D.jpg

25112012740%5B1%5D.jpg

25112012735%5B1%5D.jpg

25112012736%5B1%5D.jpg
 
Hehehe!! Wakenya wanaokumbana na haya masuala ya ubaguzi Tanzania wanafaa kuacha kulalamika ovyo, kufikia sasa kila Mkenya anafaa kuwa amejua kwamba hiyo ndio hulka ya Watanzania. Kuendelea kulalamika kwenye magazeti na mitandao haiwezi ikabadilisha chochote, ndivyo walivyo hao na waliumbwa hivyo. Tunafaa kuendelea kuboresha nchi yetu.
 
Katika enzi za knowledge economy, wewe bado unafikiria vikwazo duni sampuli hiyo???!!!

Good try.More photos of tz roads tafadhali.

Watu wajifunze na kinachotendeka Uingereza, mtikisiko wa kiuchumi ambao upo njiani kuwakuta kwa ajili ya hizi hulka za kibaguzi/xenophobic. Kwenye enzi hizi za leo, hauwezi ukawahamasisha watu wako waishi kibaguzi halafu utegemee kutoka kiuchumi.

Imagine Mkenya leo ukiingia Dar, Tanzania, halafu itokee unataka umtembelee jamaa yako Zanzibar, inabidi ulipe nauli ya boat kama mtalii wakati wanasema wao nchi moja. Wana tozo za kiajabu ajabu kwa majirani, nenda pale Ngorongoro unalipia kama Mfaransa aliyetua leo.

Tozo zao hizo hata wazungu wameanza kuwachoka, leo nimesoma mahali eti watalii 8,000 wamegeuza na kukatiza safari zao za kuingia Tanzania na kusababishia nchi kupoteza dola milioni sita. Soma hapa Watalii (wageni) zaidi ya elfu nane wakatisha safari zao kutokana na kodi
 
MK254 hamna mtalii anaulizia VAT, wanajua vp kuhusu VAT kama si propaganda za kipuuzi!?
 
Watu wajifunze na kinachotendeka Uingereza, mtikisiko wa kiuchumi ambao upo njiani kuwakuta kwa ajili ya hizi hulka za kibaguzi/xenophobic. Kwenye enzi hizi za leo, hauwezi ukawahamasisha watu wako waishi kibaguzi halafu utegemee kutoka kiuchumi.

Imagine Mkenya leo ukiingia Dar, Tanzania, halafu itokee unataka umtembelee jamaa yako Zanzibar, inabidi ulipe nauli ya boat kama mtalii wakati wanasema wao nchi moja. Wana tozo za kiajabu ajabu kwa majirani, nenda pale Ngorongoro unalipia kama Mfaransa aliyetua leo.

Tozo zao hizo hata wazungu wameanza kuwachoka, leo nimesoma mahali eti watalii 8,000 wamegeuza na kukatiza safari zao za kuingia Tanzania na kusababishia nchi kupoteza dola milioni sita. Soma hapa Watalii (wageni) zaidi ya elfu nane wakatisha safari zao kutokana na kodi
Hatutaki watalii maskini..
 
Frankly Tanzania does things in reverse psychology. Which Kenyan would be perturbed if they sold Lake Turkana as part of Tanzania to their tourists as long as they pay to access the park if any?
 
mwaswast, mpuuzi mwenzio Livale anaongelea mambo ya 2010 leo!
Livale aliuliza kiistaarabu tu nd yupo poa tu......

Wakenya wengi wanaijua Tanzania kupitia stories au ameishia dar tu hivyo, kuwaambia kiistaarab ni vyema zaidi though ninawajua trouble makers na wapo katika ignore list yangu
 
Geza nishamzoea Kaka, aweza kupa habari njema ya kuwa umeshinda millioni kwa kukuita "wewe millionaire hohehahe". Hata hakuona chini ya matamshi yangu nilisema natumai Kikwete alifanya kazi hapo kwani nilijua ni ya kitambo hio na nikakumbuka azimio la rais huyo mstaafu la kuiunganisha mikoa yote kwa hivyo uwezekano wa barabara hii kutokuwa lami nlikua nishaitilia Shaka.
 
Nawe huleta picha za miaka io hio eti barabara za sasa za northern Kenya, ukishapewa uhalisia kupitia picha you immediately start tripping and denying

But that's a good road there, may Tz keep up the work

Huu unafiki wa Wabongo ndio mimi huwa unaipa shida sana, nyie mkifanya inakua swa, wengine tukijibu mnalialia na kulalamika. Huku kutwa mnaweka mabango ya mapicha ya Turkana ya miaka ilee ya zamani, tukileta mada za mabadiliko yanayoendelea kule maeneo hayo ya Turkana mnabishia na kusisitiza kwamba hamna jipya.

Ieleweke nchi zetu hizi kwa leo zinapiga hatua kubwa sana, tulioyaona kipindi kile sio ya leo. Mwenyewe nimesafiri kwenda Ngorongoro nikitokea Arusha na kupitia Karatu miaka michache imepita. Aisei kuna safu ya hiyo barabara ilikua noma, yaani mbaya kabisa. Hata kusinzia kwenye gari ikawa shida, kama wamerekebisha leo, nawapa hongera.
 
Back
Top Bottom