Transparency International: Ufisadi umekithiri Afrika Mashariki

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mataifa mengi ya Afrika yamekuwa yakifanya juhudi za kukabiliana na ulaji rushwa. Lakini juhudi hizi zinafanikiwa?

Takwimu za hivi punde zinaonesha taswira mbaya kuhusiana na kuzorota kwa maadili na uadilifu miongoni mwa viongozi wengi wa Afrika na haswa kusini mwa jangwa la Sahara.

Takwimu za hivi punde zaidi zinaonesha kuwa ufisadi umesakama uchumi wa mataifa 40 kati ya 46 Kusini mwa jangwa la Sahara.

Katika kanda ya Afrika Mashariki, Burundi inaongoza kwa kiwango cha juu zaidi cha Ufisadi ikiorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani ikiwa na jumla ya alama 21 pekee.

Uganda na Kenya zimetoshana katika nafasi ya 139 zikiwa na alama 25.

Tanzania ina alama 30 na imeorodheshwa katika nafasi ya 117 duniani.

Rwanda ndio taifa lililoongoza katika kanda hii ya Afrika kwa kupigana na ufisadi.

Rwanda inaalama 54 na imeorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.

Botswana ndio inayoongoza barani Afrika kwa vita dhidi ya ufisadi.

Taifa hilo la kusini mwa Afrika lina jumla ya alama 63.

Cape Verde ni ya pili na alama (55), Seychelles ya tatu na alama (55), Rwanda ni ya nne na alama (54), 5;Mauritius (53)nayo Namibia ikiorosheshwa katika nafasi ya 6 na alama (53).

Mkurugenzi wa Transparency International (TI) kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara Chantal Uwimana, anasema kuwa kuanzia kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hadi kukithiri kwa mashambulizi ya kigaidi bara la Afrika linazidi kujuta kutokana na kukithiri kwa visa vya ufisadi.

''haijakuwa mwaka mzuri kwa mataifa ya Afrika na haswa katika mataifa makubwa zaidi kiuchumi barani yaani Afrika Kusini na Nigeria ambapo visa vya ufisadi vimepelekea kuibuka maandamano ya umma na vilevile badiliko la kisiasa kufuatia uchaguzi mkuu nchini Nigeria'' alisema Uwimana.

''Iwapo Afrika inataka kwa kweli kupigana vita na ubadhirifu wa mali ya umma, na matumizi mabaya ya mamlaka kwa faida ya kibinafsi sharti mataifa ya Afrika yawekeze katika jitihada za kupamabana na ufisadi .'' aliongezea.

Somalia ambayo imekuwa bila serikali ya kitaifa tangu mwaka wa 1991 ndio taifa linaloongoza kwa visa vya ufisadi.

Taifa hilo la upembe wa Afrika linashikilia nafasi hiyo kwa pamoja na taifa la kikomunisti la Korea Kaskazini.

Ripoti hiyo inasema kuwa japo serikali nyingi za Afrika zinajaribu kupunguza vizuizi vya kufanya biashara, wananchi wake hawajabadili mtazamo wao kuhusu maadili.

Takwimu hii ya shirika la TI inatathmini hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wanaolaumiwa kwa kushiriki ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Aidha pia inapiga msasa hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wafisadi.


Source: BBC
 
Kweli inauma, Afrika laana tu hamna lingine, sasa hapa kwetu Kenya hata mahakimu wanaoongoza kwa ufisadi. Anyway hongera Rwanda kwa juhudi zenu hadi mumeongoza Afrika yote kwa vita dhidi ya ufisadi.
 
Kuhusu hiyo report its true.end of January this year,kuna baadhi ya vyombo vya habari viliandika taarifa ya kampuni moja kubwa kuja kuwekeza katika ujenzi wa nyumba Tanzania. Loool nikajiuliza waandishi hawa taarifa wanapewa na nani? niliongea na CEO wa hiyo kampuni alikuwa akisikitika sana na ameamua kuacha kuwekeza hapa nchini amepeleka mradi huo wa nyumba takriban 10,000 nchi nyingine tofauti na Tanzania.
 
Back
Top Bottom