Trafiki ndio chanzo kikuu cha ajali barabarani

Trafiki ndio chanzo kikuu cha ajali barabarani

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,623
Reaction score
5,054
Habari zenu wakuu wa JF. Ni matumaini yangu kuwa mko poa kabisa. Bila kupoteza muda ngoja niingie kwenye hoja moja kwa moja.

Ni kwamba tarehe 10/07/ 2018 katika maeneo ya kimara korogwe nilishuhudia trafiki akiwa katika utendaji kazi wake wa kazi ambao ungepelekea kutokea ajali mbaya sana na watu kupoteza maisha yao kwa sababu za kizembe sana.

Ilikuwa mida ya jioni natoka kazini nilimshuhudia huyo askari akiwa anaruhu magari kupita wakati kuna kundi kubwa la wavuka kwa miguu walikuwa wanavuka. Kiukweli nilipigwa na butwaa sana ingawa nilijua kakosea kufanya hivyo kumbe ni mazoea yake maana alifanya hivyo kama mara tano hivi jambo ambalo lilipelekea wavuka kwa mguu katika kile kituo cha mwendokasi cha korogwe kuteseka sana kipindi wanavuka.

Ilifika muda wenye magari wakawa wanaonesha ustaraabu na hekima zao kwa kusimama wenyewe ili wavuka kwa miguu wapite bila kujali ruhusa ya yule askari ya kuwaruhusu waendesha magari wapite wakati kuna watu wanavuka.

Hivyo basi yule askari ingekuwa vyema sana kama angechukuliwa hatua kwa lile jambo alilokuwa anafanya bila kuzingatia wala kuwaza ni kitu gani kingetokea au huenda alikuwa anajua madhara yake ila akawa analeta dharau tu.

Naishauri mamlaka husika wamchukulie hatua yule askari kwa tukio alilofanya kwa sababu angeweza sababisha ajali kubwa sana katika eneo lile kama waendesha magari wasingetumia akili zao vizuri.

karibuni kwa maoni yako mwana JF.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom