mnyawusi
Senior Member
- Apr 1, 2012
- 169
- 254
Nimekuwa nikipanda daladala mara kwa mara katika kituo cha Makumbusho na imekuwa ni jambo la kawaida kwa askari wa usalama barabarani katika kituo hicho kuchukua rushwa kutoka kwa madereva na makondakta wa daladala zinazoingia kituoni hapo.
Ukiwa unaingia kituoni hapo kutoka barabara ya Mwananyamala,wako askari wawili kila siku wapo kwenye kona ya kuingia kituoni.Mmoja wa askari hawa anaitwa Said na kila gari linaloingia kituoni hapo hulipiga mkono lisimame pembeni na kisha kondakta kumpelekea fedha kati ya elfu mbili na elfu tatu.
Nimewahi kushuhudia mara kadhaa mazungumzo ya kondakta na dereva wanasema limekuwa jambo la kawaida kumpatia fedha askari huyo hata pasipo kuwa na kosa na wala hawapewi risiti yoyote.
Tafsiri yake ni kwamba askari huyu anachukua rushwa kutoka kwa madereva/makonda wa daladala zote zinazoingia kituoni hapo kutokea barabara ya Mwananyamala.
Kutokana na rushwa hiyo daladala nyingi hulazimika kushusia abiria hapohapo kabla ya kuingia kituoni na inasababisha usumbufu kwa abiria wenye mizigo na watu wenye matatizo mfano walemavu na wagonjwa ambao nao hulazimika kuteremka kwenye gari na gari kugeuzia hapo.
Jambo la kushangaza ni kuwa askari huyu Said na mwenzake wanafanya hivyo kila siku pasipo wasiwasi wowote na hata kuibua hisia kwamba huenda ni utaratibu unaofahamika hata na wakubwa wao huku serikali ikipiga kelele kila siku kukemea vitendo vya rushwa.
Wenye mamlaka tupieni macho hapo na kama ni halali basi watoe na risiti ili tujue fedha hizo zinaingia serikalini,vinginevyo hiyo ni rushwa tena ya mchana kweupe.