Trafiki Arusha acheni huu wizi wa mchana

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Naomba nizungumzie tabia ya trafiki wa Arusha kuweka mitego ya kupata hela mahali wanajua kabisa hakuna alama ya kumwelekeza dereva. Kwa mfano kuna trafiki wamewekeza eneo la Moshono kwenye mteremko wa kutokea Club D hadi Boma ya Siara. wanakamata magari na kuyapiga faini kwa kigezo cha kuvunja sheria za usalama barabarani wakati hamna kibao hata kimoja kinachomwelekeza dereva kupunguza mwendo. Tukiwabana kutuonyesha kibao kinachooonyesha speed limit ni 50 KPH kiko wapi wanasema "TUMIA AKILI ENEO LA MAKAZI SPIDI INAJULIKANA"then wanatutoza shs 30,000. Nataka nijue kama hii ni sawa kwani hakuna sehemu barabara za Arusha na Moshi hazipiti eneo lisilo na makazi. Na watuambie makazi ni maduka au ni nyumba za familia za kuishi. Barabara ya Arusha- Moshi , Arusha- Babati nk zote zinapita maeneo ya makazi kwa hiyo utoke Moshi hadi Arusha au Arusha Babati kwa spidi ya 50KPH?. Kitendo cha trafiki wa Arusha kutosisitiza TANROADS kuweka alama za barabarani za tahadhari na badala yake kuwatega madereva ili wapate hela nasema ni wizi na unyanganyi wa mchana kweupe. Tabia hii imewaudhi watu wengi hadi kupelekea wenye magari kuamini kuwa trafiki wanahusika kung'oa vibao elekezi barabarani ili kuwatega watumiaji wa barabara na hivyo kuwapiga fine ambazo hazijulikani zinakwenda kwa nani. Usumbufu huu ni mkubwa mno kwa maeneo ya pembezoni mwa barabara. Imefikia hatua trafiki wanajificha bondeni kwenye mteremko wa Moshono Secondary na tochi na wengine wanakaa eneo la Masai Camp. Aliye na tochi anampa signal aliyeko Masai Camp kuwa gari no.... ikamate hata kama yuko 57KPH au hata 55KPH. huu ni wizi na utendaji usiofuata kanuni ambao kwa level zote unaashiria kutafuta hela kwa nguvu na si kusimamia usalama barabara ni kupunguza ajali. Nawashauri trafik wawabane TANROADS kuweka vibao barabarani na si kuwataka wenye magari kubahatisha au kutabiri uwepo wa vibao barabarani. Sheria zote zina guideline na ili ubanwe lazima iwepo reference kuonyesha umevunja sheria ipi .Kama trafiki wanajua kutambua invisible vibao basi wao ndio wanajua viko wapi na ni nani alivyingoa, maana wasingekuwa wanajua wasingekuwa wana kaa maeneo yasiyo na vibao na kuwaaminisha watu kuwa wamevunja sheria kwa reference ambazo hawazioni zaidi ya wao trafiki kuzijua . Huu ni wizi na uonevu wa hali ya juu tunaomba mamlaka husika kuwabana hawa matrafiki waache huu uhuni. Imefika mahali trafiki akiamua uwe na kosa ni jambo rahisi na utalipa faini hata ujitahidi vipi. Hiace zao ambazo ni asilimia 90 ya zinazofanya kazi ya daladala hapa Arusha zinafanya lolote including kutanua na kusababisha jam kutoka clock tower hadi Impala lakini hawawakamati wakijua ni magari yao. Hii ni doble standard ya hali ya juu.
 
Kwa ufupi trafiki wa Arusha wananyanganya wenye magari hela kwa kuwatengenezea mazingira ya kuwakamata na kosa. Ni mfano wa refa anayetaka kuipa ushindi timu fulani lazima itashinda tu. Trafiki akiamua uonekane na kosa anafanya hivyo na hii naita ni roho ileile ya kubambikia watu makosa
 
Wajinga sana wapo mianzini wengine ukitokea sanawari kwenye mataa ukikunja kwenda stand kuu wanakushika wanakwambia umepita bila kuruhusiwa na taa wakati hakuna taa zinazoruhusu magari yakushuka stand kuu ukitokea sanawari
 
tatizo ni watanzania kukubali jeshi la usalama barabarani kujisifia kwa kukusanya mapato badala ya kupunguza ajali.
 
Back
Top Bottom