Trafic Tochi

Trafic Tochi

msembezu

Senior Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
179
Reaction score
29
Siku hizi trafic wanapiga picture kwa nyuma je hii ni halali?
 
Siku hizi trafic wanapiga picture kwa nyuma je hii ni halali?

Ni halali. Ila wakikusimamisha mbele wadai ushahidi, na usikubali kuwapa lift mrudi kule walikomweka mtu wa kamera, hiyo sio kazi yako.

Siku moja tulitaka kumpopoa vibao askari wa kamera kwa sababu huwa wanavaa kiraia na kujificha. Tukamwambia tunajuaje kama sio kibaka anavizia magari ya kuteka na kuwaarifu wenzake huko mbele? Alifanya haraka sana kutuonyesha vitambulisho, lakini tulimwambia aondoke pale, na kama yuko kazini akavae uniform!
 
Sio kwa nyuma,zile machine zao zinapiga mpaka mbele na kama ulikuwa karibu zaidi hata dereva unaweza kujiona....Mie walishawahi kunipiga tochi nikajiona .....Ndo machine mpya hizo ndugu yangu
 
Hawa jamaa siku hizi wanabambikia watu baada ya kujua watu wanazingatia sheria na wanapigia nje ya kibao cha 50. Mimi kuna trafiki alidai nimetembea 69 km nda ya eneo la 50, sikukubaliana nao kwa sababu niko makini na nilikubali kurudi ilipo kamera na niliwaumbua kukuta anaepiga yuko nyuma kabisa ya kibao cha 50 na pia picha inaonyesha kabisa mandhari hiyo , hapo walichanganyikiwa na kuanza kujikanyagakanyaga tu. Kwa sababu niliamini gari yangu iko full masinondo, niliwachenjia kuwa ushahidi wa picha hiyo ambayo niliwarekodi kwa simu wakiniomba radhi tuyapeleke mahakamani kama wao walivyotaka kunipeleka mahakamani. Walipagawa kabisa mpaka leo ni marafiki zangu. Madreva wenzangu msikubali kirahisi kulipa kama una uhakika ulifuata sheria.
 
Back
Top Bottom