Kwa mtu anayetumia barabara ya Nyerere huenda atakuwa ameliona au ameshawahi kukutana na dhahma hii hasa madereva. Unapotokea uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere unapofika eneo la vingunguti utakuta alama za zebra ambazo huonyesha eneo ambalo waenda kwa miguu wanatakiwa walitumie kuvukia ambapo mbele yake kuna taa za kuongozea magari.
Eneo hilo askari wa usalama barabarani wanalitumia vibaya kuwaonea wananchi ambao wanatumia barabara hiyo kwani endapo utafika eneo hilo la kuvukia watu ukasimamisha gari na baada ya kujiridhisha ukaaamua kwenda mbele ukikuta taa haziruhusu kupita basi ujue trafiki watakuja na kukutoa nje ya barabara na kukupiga faini huku wakijua wazi kuwa wanakuonea.
Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam tafadhari umulike eneo hili kwani hawa askari pamoja na ukweli kuwa wanaleta hizo faini kwako lakini nyingi hazijapatikana kwa halali na ni za uonevu. Ni kweli kuwa huenda sifa itapatikana mkitoa hesabu ya makusanyo ya faini ila hela ya dhulma italeta laana katika nchi pamoja na askari anayeisimamia. Ninaomba sana mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa mkoa Paulo Makonda afanye utafiti wake eneo hili ili aone uonevu unaofanywa na hawa askari ambao wamekaa eneo hilo kuonea watu ambao wengine hawana kosa walilolifanya.