Traffic Mbeya huu ni wizi wa wazi kabisa

Ohooo

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
807
1,084
Sote tunajua kua kazi kubwa ya askari wa usalama barabarani ni kulinda watumiaji wa bara bara pamoja na vyombo vitumiavyo barabara hizo kama magari, pikipipiki na vyombo vyote vya moto na visivyo vya moto.

Wanahakikisha kua vyombo vipo imara na pia watumiaji wanatumia barabara kwa usahihi bila kuhatarisha maisha yao na ya wengine.

Lakini hali hii ni tofauti kabisa na askari wanaokua eneo la Izumbwe barabara ya kutoka Mbalizi kwenda umalila katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini. Kama RTO wa mbeya huna taarifa hizi please ebu tumbua Jipu hili au kama ni wewe unawatuma basi nawe unafaa kutumbuliwa.

Hawa askari hukaa tu pale Izumbwe na kusimsmisha magari halafu hukusanya hela tu bila kujali kama gari husika likoje wao ni hela tu.

Mbaya zaidi hawana hata stakabadhi yoyote kuthibitisha malipo hayo. Haijulikani hua wanapewa kiasi gani lakini inaonekana kila gari linalopita pale hutozwa si chini ya sh 2000 kwa kila gari.

Sasa sijui hizo tozo ni faini au nini maana hupiti pale bila kutoa hela kwa askari hao. Nadhani wahusika mtasikia hili na kama hamtajirekebisha msubiri kutumbuliwa.
 
hii watu bana napenda kula siku yote, hata natumbua leo keso natoka pele ingine baadae nakua jipu kuba !
 
Back
Top Bottom