TRA yavuka lengo, Yakusanya trilioni 1.4 kwa mwezi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
PIX 1.jpg

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .

Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao.

Chanzo: Michuzi
 
g
View attachment 315193

Goodnews. lengo liwe siku moja tujitegemee asilimia mia. kuombaomba ni aibu.
 
Kazi njemaa. Ilakipomo kizuri ni muendelezo wa makusanyo baada ya miezi minne.
 
Bado,TRA ina uwezo wa kukusanya zaidi ya Tri.2 if well managed.Kilichofanywa huko nyuma ilikuwa underestimation ya makusudi ili watu waweze kula.Tulilizungumza sana hili lakini kwa kuwa mamlaka iliyokuwepo ilikuwa inafaidika na underestimation yenyewe,we were never taken seriously.Very sad indeed.
View attachment 315193
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .

Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao.

Chanzo: Michuzi
 
Sawa hiyo ilitegemewa hasa ukizingatia kuwa ni makusanyo ya mwezi December (mwezi wa hela) na huu ni mwezi wa mwisho kwa wafanyabiashara wenye malimbikizo ya kodi ya mwaka mzima kutakiwa kulipa lodi zao.

Tunataka habari hizi za matrilioni ziendelee mpaka mwezi huu wa January mpaka December. Hapo tutatembea kifua mbele kwamba tunasonga mbele, vinginevyo ni blaablaa kama za kipindi cha Jk tu..!!

Anyway mwanzo mzuri tusonge mbele

BACK TANGANYIKA
 
Last edited:
Hizi ni kwa sababu ya zile walizokwepa pamoja na Fine au hizi ni zile za makusanyo ya kawaida kwa mwezi ? Sababu kama ni Fine na marejesho ya wezi basi huenda makusanyo yakapungua ila kama ni makusanyo ya kawaida ni vema na hii itakuwa source of income nzuri
 
Mimi.hizi story zinanichosha kweli.maisha magumu balaaa...mimi kama mwananchi wa kawaida natamani unafuu wa maisha niweze kula milo mitatu.mishahara midunchu bado makidamakida sana yanachezwa hapa
Nani kakwambia serikali kazi yake kulisha watu!?

Wewe endelea kufanya kazi, kuwa mbunifu na ujiendeleze. Usitegemee serikali ikuingizie pesa mfukoni. Kwanza misingi ya uchumi inapiga marufuku kuongeza mishahara hovyo hovyo.

Serikali kazi yake ni kuweka mazingira wezeshi ya watu kujifanyia shughuli zao na pia kutoa huduma za kijamii...Na kwa makusanyo haya ya kodi ndio utekelezaji wa hili jukumu utafanywa kwa ufanisi zaidi.
 
Back
Top Bottom