TRA yavuka lengo la makusanyo wa Mapato mwezi Mei 2016

TRA yavuka lengo la makusanyo wa Mapato mwezi Mei 2016

NYAMY

Member
Joined
Feb 16, 2016
Posts
14
Reaction score
32
Mamlaka ya mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi za kitanzania trilio 1.032 katika mwezi May ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya kiasi cha trilion 1.025 katika mwezi huo.
===========================

Ikiwa imewekewa lengo la kukusanya Sh12.054 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Mei 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kufikia malengo kwa kukusanya Sh1.032 trilioni kwa kipindi cha mwezi uliopita, ikiwa ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo lililowekwa.

Makusanyo hayo yanaifanya Serikali ya Awamu ya Tano iliyoingia madarakani Novemba 5, 2015 kukusanya zaidi ya Sh6.567 trilioni katika kipindi cha miezi mitano. Takwimu zinaonyesha kwamba kuanzia mwezi Desemba, TRA haijakusanya mapato chini ya Sh1 trilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema lengo lao kwa mwezi uliopita lilikuwa ni kukusanya Sh1.025 trilioni na kwamba, kuanzia Julai 2015 hadi Mei 2016 wamekusanya Sh11.956 trilioni.

“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha na kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo, hususan katika mipaka,” alisema Kidata.
 
Imetolewa na idara ya huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA.Hii ni kama ilivyoripotiwa na michuzi blog.
 
Safi
But wajitaidi kuongezeka uko kuendane na wepesi wa maisha
Kichwa nyndo si lazima kuendane na wepesi wa maisha yako kwani serikali haijui namna maisha yako yanakuwa magumu. Pengine huzalishi kwa tija, huna utaratibu wa kuweka akiba na kuwekeza kidogokidogo, pengine umekusanya wategemezi wengi kwa kuzaa kama uko mashindanoni na upuuzi mwingine. Aliyekukaririsha haya anakuchelewesha sana kusubiri kuwa ipo siku pato litaongezeka na wewe kwako zikajaa abadani. Rekebisha maisha yako mwenyewe
 
Wawe wanatutangazia malengo kabla ya mwezi ili tuwe na kumbukumbu sahihi juu ya target zao, mfano mwezi juni wanataraji kukusanya shilingi ngapi?
 
Kichwa nyndo si lazima kuendane na wepesi wa maisha yako kwani serikali haijui namna maisha yako yanakuwa magumu. Pengine huzalishi kwa tija, huna utaratibu wa kuweka akiba na kuwekeza kidogokidogo, pengine umekusanya wategemezi wengi kwa kuzaa kama uko mashindanoni na upuuzi mwingine. Aliyekukaririsha haya anakuchelewesha sana kusubiri kuwa ipo siku pato litaongezeka na wewe kwako zikajaa abadani. Rekebisha maisha yako mwenyewe
Tatizo ni nini mkuu?
 
Lengo

(Trilioni) Makusanyo halisi

December 2015 1,346,690.4 1,403,189.8

January 2016 1,059,863.9 1,079,993.2

February 2016 1,028,379.4 1,040,620.8

March 2016 1,302,482.3 1,316,072.4

Jumla ya makusanyo hadi sasa kuanzia mwezi July 2015 ni TRILIONI 9.88 ambayo ni 99% ya lengo la makusanyo ya TRILIONI 9.98 ya miezi tisa kwa mwaka wa fedha 2015/2016

ULIIKOSA YA RA
 
Mamlaka ya mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi za kitanzania trilio 1.032 katika mwezi May ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya kiasi cha trilion 1.025 katika mwezi huo.


exchange impact bana!

look at the rough estimates below.....

May 29 2015: shs 2,007/$ (budget)
May 31 2016: shs 2,173/$ (actual)
variation: 8.3%
translates to a shs 54 billion deficit (within a biased margin of error of -3% to the exchange variation)
so actual income should be around shs billion 970.
 
Back
Top Bottom