TRA Yamva Mama Salma Kikwete

Status
Not open for further replies.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inakaribia kupiga mnada baadhi ya mali za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambayo Mwenyekiti wake ni mama Salma Kikwete, mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Raia Mwema linafahamu.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka 20 kwa taasisi ya mke wa rais kutangazwa hadharani na TRA kama sehemu ya wateja ambao mali zao ziko hatarini kupigwa mnada kutokana na madai ya kodi. Miaka hiyo 20 inajumuisha ile ya utawala wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na utawala wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo gazeti hili inazo, tayari WAMA inafanya jitihada za kunusuru hali hiyo kwa kuwasiliana na viongozi mbalimbali walio madarakani hivi sasa.

Tayari TRA imetoa taarifa kwa vyombo vya habari inayoeleza kuhusu mzigo huo uliokwama bandarini na imetaka wahusika wawe wamelipa deni kabla ya mapema mwakani ambapo vitapigwa mnada.

Hadi sasa, mzigo ambao umetangazwa rasmi na TRA kuwa unamilikiwa na taasisi hiyo inayojihusisha na masuala mbalimbali ikiwamo kusaidia watoto wa kike kupata elimu bora ni vitabu kutoka Japan.

Kwa mujibu wa sheria za masuala ya forodha hapa nchini, mzigo unaweza kukaa bandarini kwa muda wa siku 21 na ikizidi hapo huwa kuna faini mbalimbali na mwishowe ndiyo uamuzi wa kupiga mnada hufikiwa.

Wiki iliyopita, katika taarifa rasmi iliyotolewa na TRA na kuchapwa katika gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), WAMA pamoja na taasisi nyingine mbalimbali za kidini na ofisi za balozi za nchi za nje nchini vilitajwa kuwa katika tishio la kupigwa mnada kwa mali zake zilizotajwa.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu, Mkurugenzi wa Elimu kwa Huduma za Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema ni kweli kwamba kuna mali za WAMA ambazo zinaweza kupigwa mnada endapo hazitalipwa kufikia tarehe ya mnada.

“Kwanza, la kwanza kabisa ambalo jamii inatakiwa kujua ni kwamba si kwamba hizi mali za taasisi mbalimbali na watu binafsi zilizotangazwa kupigwa mnada zitauzwa kesho. Hapana.

“Tangazo letu lile linamaanisha kwamba wale wote ambao hawajalipia mizigo yao kama sheria inavyotaka, basi wailipie. Kama itafika Januari 5 na mhusika atakuwa hajafanya hivyo, basi hapo ndiyo tunaweza kuuza.

“Hivyo tangazo lile lisichukuliwe moja kwa moja kwamba ni la kupiga mnada. Unajua kuna sababu nyingi za watu kutolipia mizigo yao na si kuwa wote wanafanya makusudi.

“Ndiyo sababu tumetoa muda mrefu kwa wahusika kabla ya kufanya mnada. Kati ya leo hadi tarehe 4 Januari, kama mwenye mali akija na kulipia kiwango kinachotakiwa, basi atachukua mali yake. Kuna muda mrefu sana kati ya sasa na Januari 5 mwakani,” alisema Kayombo.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu wiki hii, Katibu Mtendaji wa WAMA, Daudi Nassib, alikana kuwako kwa mzigo huo unaoshikiliwa na TRA tayari kwa ajili ya kupigwa mnada.

Alipoambiwa na Raia Mwema kwamba mzigo unaosemwa ni ule wa vitabu vya fasihi kutoka Japan, Nassib alisema mzigo huo ulishatolewa bandarini zamani na kugawiwa.

“Kama mzigo unaouzungumzia ni ule wa katoni za vitabu kutoka Japan, basi mzigo huo tayari tulishautoa bandarini. Hakuna mzigo wa aina hiyo unaoshikiliwa na TRA,” alisema kwa kujiamini.

Hata hivyo, TRA imesisitiza kwamba bado mzigo huo hajalipiwa.

Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja sasa, kumekuwa na taarifa kutoka katika duru mbalimbali za kiserikali na TRA kwamba kuna mzigo mkubwa wa WAMA unashikiliwa bandarini kwa sababu haujalipiwa kodi.

Taarifa za awali zilieleza kwamba katika miaka ya nyuma, WAMA ilikuwa ikipata misamaha ya kodi lakini katika utawala wa sasa wa Rais John Magufuli, baadhi ya misamaha ya kodi kwa taasisi na makampuni imeondolewa.

Kwa mfano, katika orodha ya taasisi ambazo mali zake zilizoko bandarini ziko hatarini kuuzwa ni pamoja na taasisi za kidini ambazo zilikuwa na misamaha katika miaka ya nyuma.

Alipoulizwa na Raia Mwema endapo kuna mzigo mkubwa zaidi wa WAMA umeshikiliwa bandarini tofauti na uliotajwa na TRA, Nassib alisema kwamba hawezi kuzungumzia mzigo mwingine wowote zaidi ya huo ambao mamlaka hiyo imeuweka hadharani.

“ Kwa mzigo huo ambao unasema umewekwa hadharani na TRA, naweza kukwambia kwamba tumeshautoa. Ni mzigo mdogo tu na hata kodi yake kwa ujumla haizidi shilingi laki tatu za Kitanzania. Siwezi kuzungumzia mambo ya mizigo mingine ambayo haijatajwa,” alisema.

Wakati alipoulizwa kuhusu uwepo wa mzigo mkubwa wa WAMA ambao umeshikiliwa bandarini mwezi mmoja uliopita, Kayombo wakati huo aliomba kufanya uchunguzi ili kujua kama kuna ukweli wowote kwenye hilo.

Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeambiwa kwamba mama Salma mwenyewe alikuwa akijitahidi kutumia ushawishi wake wa kisiasa katika ngazi za juu kujaribu mizigo hiyo ya WAMA iruhusiwe kutoka bandarini.

“ Mama Salma amepambana kwelikweli kujaribu kusaidia mizigo ya WAMA itoke bandarini. Tatizo ni kwamba hivi sasa mambo ya misamaha ya kodi yanapigwa vita na kila mtu anatakiwa kuchangia, Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake kutoka WAMA.

Katika mazungumzo na gazeti hili, Nassib alikiri kwamba wakati mwingine asasi zisizo za kiserikali kama WAMA huingia katika kufanya malipo ya kodi kwa vitu ambavyo vinatumika kwa kutoa elimu kama vile vitabu na kompyuta.

“ Unajua haya mambo ya kuchelewa kulipa yapo. Lakini hivi sasa tuna uzoefu kwa sababu tumeanza kulipia kodi muda kidogo. Tunalipia kodi hata kwa vitu kama kompyuta na vitabu ambavyo wanatumia watoto hawa kujielimisha. Lakini ndiyo taratibu na lazima zifuatwe,” alisema.

WAMA ni taasisi ya pili isiyo ya kiserikali kuanzishwa na mke wa Rais, baada ya ile ya Fursa Sawa kwa Wote iliyoanzishwa na mke wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, mama Anna.

Mke wa Rais Magufuli, Janeth, hajaanzisha taasisi ya namna hiyo hadi sasa na duru za Ikulu jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa kwa sasa hana mpango wa kuanzisha taasisi ya namna hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya WAMA, taasisi hiyo ina bodi ya wakurugenzi yenye majina ya watu maarufu kama vile mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina, Mweka Hazina wa CCM, Zakhia Meghji na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Marekani, Mwanaidi Maajar Sinare.

Wanawake wengine maarufu wanaotajwa kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Sofia Simba, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Blandina Nyoni na mke wa Rais wa Zanzibar, mama Mwanamwema Shein.

WAMA ilianzishwa Oktoba mwaka 2006, mwaka mmoja baada ya Kikwete kuingia madarakani kama Rais wa Tanzania; ikiwa na lengo la kusaidia wanawake, watoto wa kike na watu wengine wa makundi maalumu katika masuala mbalimbali kama vile elimu na afya kwa minajili ya wao kuja kutoa mchango katika maendeleo ya nchi


Chanzo: Raia Mwema

=========

Hii habari imekanushwa na Ikulu, zaidi soma=>Ikulu yakanusha taarifa ya mali za taasisi ya WAMA inayoongozwa na mama Salma Kikwete kupigwa mnada
 
wajinga waliwao hapa nimwendo wa propaganda na ulaghai

Tunadanganywa na kutapeliwa ......hata tra?
 
Huo ni uongo na haiwezi tokea,ninachoona ni propaganda tu.
 
Kwani yeye sio sehemu ya wale wanaolindwa?.Nitakuwa wa mwisho kuamini hi hadithi.
 
Hii serikali kwanini inafurahia kila mtu kufirisika,kila taasisi kukwama why?.....

Up ndio uzalendo?......
 
Ndioooooo wamfunge kabisa na yeye aonje maisha ya kishetani!
 
Hizi taasisi mara nyingi hazifanyi kazi kwa malengo kusudiwa, angalia hata viongozi wa hiyo taasisi wamekaa kipigaji tu.

Salma Kikwete,Zakhia Meghiji,Sofia Simba,Rejina Lowasa, Blandina Nyoni nk.

Mara nyingi hata mizigo wanayoingiza haiendani na taasisi husika, wafanyabiashara wengi wanapitisha mizigo yao humo kukwepa kodi.

Bora serikali imeamua kusimamia ukweli kwenye hili.!
 
"Sitafukua makaburi". Kumbe alimaanisha (pengine) yenye masilahi yake: kama vile makaburi ya DSM ferry, nyumba za serikali, mikataba ya ujenzi n.k.
 
Hili si UONEVU wala witchhunt bali ni kwa NIA nzuri tu. Sheria ni sheria. Haingalii cheo cha mtu. Ndio maana wahenga wakasema sheria ni MSUMENO!
Kulipa KODI ni jukumu la kila mwananchi.
 
Mama zakiah ampe mama salma chupa ya maji nae anywe maji.
 
Bora serikali imeamua kusimamia ukweli kwenye hili.!
Kama WAMA ilikuwa hailipi kodi ipaswavyo (pale wanapofanya kinyume na malengo ya taasisi), basi wahusika wachukuliwe hatua, na siyo kulalamika tu!

By the way, haya makaburi yanavyofukuliwa selectively, kunafanya rais aonekane ana chuki na visasi dhidi ya watu fulani. Yeye alishasema hafukui makaburi, lakini tumeshaona Sumaye na sasa Bi Salma wakipata shuruba!
 
Hivi yale makontena ya HSC aliyozuia Mwakyembe akiwa waziri wa uchukuzi kwa kutolipiwa kodi na badala yake akapigwa mkwara na kontena zote kutolewa tena usiku sijui , Kwanini Mwakyembe asilianzishe sasa hivi kuhusu hilo swala na serikali yetu ya sasa inapambana na ufisadi kweli kweli ?

Au ni janja ya toto tu ? Ndio maana makaburi hayafukuliwi tunahangaika na wenye ndoto zao
 
Tumeitaka wenyewe,chaguo letu milele waache waisome namba__#Kunywamajimamasalma.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…