TRA yakamata magari ya TFF

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mamlaka ya Mapato Tanzania imekamata magari yote ya TFF kwa sababu ya kutokulipa kodi, wanadaiwa 1.11 bilioni

Awali walikuwa wanadaiwa 1.8 bilioni.
 
Wanatafuta hela ya kufidia MCC, tutegemee kukamatwa kwa mali za NGO's mbalimbali
 
TFF ni jipu kuu, kodi hawalipi, jana nimesikia star tv Kocha wa taifa stars hajalipwa miezi 8 mshahara wake. Wakati kodi inakatwa kila mechi zinapochezwa. Kwa upumbavu huu wa TFF ni heri kulipa azam tv uangalie mechi kuliko kwenda uwanjani ulipe kiingilio,ukatwe kodi afu kodi isifike sehemu husika.
 
Kama hizo pesa za kuuza magari hazitotosha kulipa deni wanadi majengo ya TFF na uwanja wa Karume wakiona havitoshi, wasimame magetini kila Taifa Stars inapocheza ili tuone ujanja wa Malinzi. Tumeshamchoka!
 
Hapa wasimame mlangoni kwenye gemu zote kuanzia za kimataifa na za ndani ya ligi.. Dadeki kama hatalipa mwenyewe hio pesa
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania imekamata magari yote ya TFF kwa sababu ya kutokulipa kodi, wanadaiwa 1.11 bilioni

Awali walikuwa wanadaiwa 1.8 bilioni.
Hivi TFF wana magari mengi sana au wana magari ya kifahari sana? Kodi peke yake ni bl 1.11?
Je yamekamatwa magari mangapi?
 
Hapa wasimame mlangoni kwenye gemu zote kuanzia za kimataifa na za ndani ya ligi.. Dadeki kama hatalipa mwenyewe hio pesa
Wasisahau kuzikomalia na zile zinazotoka FIFA! Lazima Malinzi anyoroke, kila siku balaa, mara kodi mara upangaji wa matokeo mara kuvuruga ratiba na haishi kulalamika ohhh kuwa watu JF hawaninipendi. Sasa nani ampende wakati anadidimiza soka na hatuoni maendeleo tangu ameingia madarakani.
 
kuna taasisi au mashirika hapa tz yatapata tabu sana maana walikuwa wanafanya wanavyotaka wengne had hum wapo .yaan mpaka sasa hawaelew kinachoendele kama utan vile nawaomba wabadilike tu.
 
Kama hizo pesa za kuuza magari hazitotosha kulipa deni wanadi majengo ya TFF na uwanja wa Karume wakiona havitoshi, wasimame magetini kila Taifa Stars inapocheza ili tuone ujanja wa Malinzi. Tumeshamchoka!
Huyu Jamal Malinzi kwa nini asitumbuliwe tu aiseee.

Kwanza kaifanya TFF kuwa genge la migogoro isiyoisha kila siku
 
TFF ni jipu kuu, kodi hawalipi, jana nimesikia star tv Kocha wa taifa stars hajalipwa miezi 8 mshahara wake. Wakati kodi inakatwa kila mechi zinapochezwa. Kwa upumbavu huu wa TFF ni heri kulipa azam tv uangalie mechi kuliko kwenda uwanjani ulipe kiingilio,ukatwe kodi afu kodi isifike sehemu husika.
kweli ni bora uone kodi yako inaenda kwenye mikono salama
 
Huyu Jamal Malinzi kwa nini asitumbuliwe tu aiseee.

Kwanza kaifanya TFF kuwa genge la migogoro isiyoisha kila siku
Kama kuna watu wanaoniudhi ni hawa watu wa FIFA, kwenye katiba za vyama vya soka kuna vipengele vinavyowalinda sana. Ukiwagusa, mbio saana kuelekea Zurich, huko huyo Bwana Malinzi anaulinzi wa kufa mtu. Humtoi na soka halichezeki na mwisho wa siku yeye atawashinda. Hicho ndicho anachoringia. Kama ulisikia juzijuzi alitaka kuchomekea kipengele cha kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu.
 
Back
Top Bottom