TRA yaidai tanesco bilioni 4/-

CPA

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
809
354
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 4 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za kodi ya mitambo ya kuzalisha umeme iliyokwama katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mradi wa uzalishaji wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi, Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Deo Ngalawa, alisema kuwa mitambo hiyo iliingizwa nchini ili kuongeza uzalishaji wa umeme.

Alisema hadi sasa mitambo hiyo imekwama baada ya Tanesco kushindwa kulipa deni la kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Tanesco inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na TRA, deni hilo linatokana na kukwama kwa mizigo ya kuzalisha umeme, ikiwamo mitambo na jenereta kutoka nje ya nchi, jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma uzalishaji wa umeme,” alisema Ngalawa.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Uwekezaji wa Tanesco, Khalid James, alisema mradi wa Kinyerezi unatarajiwa kuzalisha megawati 240 za umeme, hivyo kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo.

Alisema mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 1,700, lakini Tanesco wanazalisha megawati 1,366, kutokana na hali hiyo, kumalizika kwa mradi huo kutasaidia megawati 1,521.

Chanzo: http://mitandaoni.co.tz
 
Watu hawajielewi kweli!hivi hiyo billioni 4 na effects za hiyo mitambo ya kuzalishia umeme vinafanana kweli?hivi watu wenye akili kweli wanaweza kukwamisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa billioni 4?##BORA BASHITE
 
Muda si mrefu wote watakanusha au tutaona picha za kupongezana kuwa wamepunguza angalau bilioni 3! Kama deni la Zenji! Bongo tambarareee
 
Kwakua siku hizi ni mwendo wa visasi, Jumatatu utasikia 'Tanesco waidai TRA malimbikizo ya umeme Bilioni 12, deni la tangu 2005'
 
Back
Top Bottom