TRA Watoa namba za simu kusaidia wananchi wanaonyanyaswa na wafanyakazi wenye NYODO,....

evansGREATDeal

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
4,013
2,331

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.

Akiongea na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.

“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa,
wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu ktk 0689122515 au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0689122516
na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi effective.

Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.

TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani,imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.

Haya mambo mpaka Rais aongee ndo myaone?
 
haya mambo mpaka jpm aongee ndo watu watoe matamko????.,.kwelin tutafika???
tatizo watanzania sio wabunifu,..
 
Kufanya kazi kwa upepo ndio matokeo yake haya. Hakuna standard practise ambazo zina iguide serikali katika kutekeleza majukumi yake. Kila presda anakuwa na stile yake maana akitoka huyu akaja mwingine we go back to sq 1
 
haha tz,..bhana,...
tatizo systems mkuuu
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.

Akiongea na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.

“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa,
wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu ktk 0689122515 au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0689122516
na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi effective.

Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.

TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani,imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.

Haya mambo mpaka Rais aongee ndo myaone?

Siku zote hizo yalikuwa wapi haya manyang'au?! Watu tumefyonzwa mpaka damu!!
 
Back
Top Bottom