Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,331
- 3,487
Ukweli Imekuwa Ni Kero Sana Kwa Wafanyabiashara Hasa Alipokazia Mh Rais Magufuli Kuhusu Ukusanyaji Wa Kodi. Wafanyakazi Wa Tra Wamekuwa Mbogo Na Hawataki Mjadala Na Mfanyabiashara Anayekwenda Kwao Kukadiriwa Kodi. Wanadai Wanafanya Kazi Under Pressure Kufikia Tu Wanachoita Target Bila Kutazama Mgeni Na Mzoefu Kwenye Biashara. Hawahangaiki Kutoa Elimu Ya Kutosha Kuhusu Ongezeko La Kodi. Mh Rais Alitafakari Hili Mara Mbili Kuliko Kupata Tu Sifa Ya Kuongeza Kodi. Watazame Mianya Na Vyanzo Vipya Vya Mapato Kuliko Kukabana Na Wafanyabiashara Ambapo Mwisho Wa Siku Watatengeneza Business Terrorists. Watu Ambao Wataichukia Sana Tra Pamoja Na Wafanyakazi Wake, Na Watafanya Kila Mbinu Kukwepa Kodi. Natoa Wito Huo Waraka Mpya Wa Kodi Utazamwe Tena Na Kufanyiwa Marekebisho Ili Pawepo Na Ushirikiano Usio Na Mashaka Kati Ya Tra Na Wafanyabiashara