TRA watawasababishia watanzania msongo wa mawazo

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
TRA wanaweza kuwasababishia watanzania msongo wa mawazo na sasa#hivi kazi yao ni kupita kwenye biashara za watu na kuwaandikia makosa na faini, bila kujali ukubwa wa biashara hawana muda wa kuangalia ukubwa wa biashara na hawaangalii mfanyabiashara anamiliki mtaji kiasi gani!

Namshauri waziri wa wizara ya fedha,pamoja na kamishina mkuu wa TRA kufuatlia hili zowezi kwa makini sana, wajitahidi sana kuwa makini kwenye hili zoezi.

Wasipokuwa makuni wataongeza umasikni zaidi kwa watanzania wenye biashara ndogo ndogo.

Nawasilisha
 
Kweli kabisaa naona mwenye vibanda wanavyopata shida huku mtaanii wakisikia TRA wamefika
 
Nitakumbuka kauli ya mwalimu, ukiona serikali inaenda kudai mpaka kwa wamachinga na kuachwa mapapa hiyo ni corruption's government
 
Swali je wanaotozwa hizo kodi wanazo fedha la kulipa hiyo kodi wanayotozwa?unaweza kuwa na nia nzuri ya ukusanyaji wa kodi lkn ukaenda kukusanya sehemu isiyo sahihi
 
Hebu tupe uzoefu wako wewe katika kuhakiki matumizi ya kodi yako, mpaka sasa umeshachukua hatua ulipogundua kuwa kuna matumiz mfano ya magar ya kifahari.

Katika nchi ambazo watu wanoana kulipa kodi kama adhabu tuna safari ndefu. Lakini sisi wenyewe ni kwanza serikali haijafanya hiki au kile. Serikali bila kukusanya kodi si serikali ni usanii.

Tulipe kodi harafu tuhakikishe inatumiwa vizuri
 
Huku sio kulipa kodi, ni kukamuliwa kodi...
 
Haileti mantiki kumdai mtu kodi millioni 600 wakati anamtaji wa million 10, its shear nonsense!
 
Bank tunaweka pesa zetu nyingi kuliko tunazolipa TRA, bank wanazifanyia biashara wanapata faida na makato ya kila muhamala wanakata na makato ya mwezi pia, bank wana ushawishi na lugha rafiki. TRA wanafanya kazi kama maadui, hawana ushawishi wala maelewano, wao ni kutisha tu watu na kuwatoza pesa nyingi kwa kosa dogo, wakija dukani wanakuhoji kipolisi na kutaka kunyenyekewa na kuabudiwa.
 
TRA wanaweza kuwasababishia watanzania msongo wa mawazo na sasa#hivi kazi yao ni kupita kwenye biashara za watu na kuwaandikia makosa na faini, bila kujali ukubwa wa biashara hawana muda wa kuangalia ukubwa wa biashara na hawaangalii mfanyabiashara anamiliki mtaji kiasi gani!

Namshauri waziri wa wizara ya fedha,pamoja na kamishina mkuu wa TRA kufuatlia hili zowezi kwa makini sana, wajitahidi sana kuwa makini kwenye hili zoezi.

Wasipokuwa makuni wataongeza umasikni zaidi kwa watanzania wenye biashara ndogo ndogo.

Nawasilisha
Mkuu !! wasema watasababi... ? wameshapelek watu wengi ICU na mahospitali kujitibu BP na stresses.. yaani madeni yamewasakama wananchi na hakuna jinsi..wala njia ya kutatua presha zao!!
Hapo peke ni kutesana na kujinyanyapa... ila wengine wachache wana siasa na maTRA kwao ni kuchuma noti....
God forbid... hali siyo ya kuridhisha kbs!!
 
Mpaka leo hujui wajibu wako kama mlipa kodi?
Wajibu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara ndogo ambao wanastahili kupewa support na serekali ili watozwe kodi ndogo ili waweze kupanua biashara zao,sio kuwakimbiza kama kuku wa kienyeji anapotaka kuchinjwa,nafikiri nimekujibu vizuri,keti chini tafakari.
 
Hebu tupe uzoefu wako wewe katika kuhakiki matumizi ya kodi yako, mpaka sasa umeshachukua hatua ulipogundua kuwa kuna matumiz mfano ya magar ya kifahari.
Wewe ndio utaweza KUHAKIKISHA kodi inatumiwa vizuri na haifujwi,au ukisha kunywa gongo ndio utapata ujasiri wa kuhakikisha unawakamata majizi yote Serikalini na kuwapeleka kwenye mahakama yako kule kwa muuza gongo?
 
Gongo ndo nin mkuu? Halafu sijaelewa logic behind ur quote, would plz be straight!
 
Back
Top Bottom