namraroh
Senior Member
- Sep 9, 2010
- 114
- 125
Nawasalimu wote kwa jina la aliyetuumba na kutupa uzima na afya tele. Napenda kuwashirikisha katika jambo moja ambalo kwa muda mrefu limekuwa likinitatiza pasipo kuwa na majibu ya uhakika.
Naomba wajuzi wa mambo ya kodi haswa kodi zetu ambazo tunatozwa na mamlaka yenye dhamana ya kukusanya ushuru, naongelea TRA na sio PRA (Police Revenue Authority) ahh hapo inabidi ushangaa kidogo lakini kama ni mkazi wa Dar es Salaam najua unatambua kabisa kwamba hawa jamaa pamoja na kazi zao nyinginezo nao wamekuwa watoza ushuru wazuri.
Nirudi kwenye mada, kwa muda mrefu nimeshindwa kutambua ni kigezo gani wenzetu wa TRA wanatumia kutoza ushuru wa bidhaa mbalimbali, kwa mfano imekuwa kawaida kwa akina mama wengi kwenda Uganda kuchukua bidhaa na kuja kuziuza humu nchini, kumbuka bidhaa hizo zinapita bandari ya Dar es Salaam, lakini bado bei yake ni rahisi kuliko ya bidhaa zinazoingia moja kwa moja katika nchi yetu. Achana na bidhaa hizo, kuna vitu mbalimbali, kwa mfano mafuta ya kula, petrol na kodi za magari zote ni za ajabu ajabu, sasa najiuliza hii dhana ya uchumi wa viwanda na kuwapeleka watanzania katika uchumi wa kati kweli ni dhamira ya serikali au ni wimbo wa kisiasa ambao tumezoeo tumezoea kusikia mara mara!
Naamini kabisa kwamba uchumi imara unajengwa na sera imara na za uhakika za kodi katika nchi husika, kama kodi hazitabiriki ni vigumu sana kwa wawekezaji kuwa na imani na nchi husika hivyo kukosa fursa ya kuwekeza. Mafuta ni nguzo imara ya uchumi kwani ndio nishati kubwa inayohitajika kwa ajili ya kujenga uchumi imara!
Napata wakati mgumu sana kuamini kwamba wasaidizi wa Rais wanafanya kazi zao kama inavyopaswa, je TRA haina idara ya utafiti ambayo ingeweza kutambua athari ya kutokuwa na kodi inayoendana na uhalisia au maziingira yanayotuzunguka, hatuwezi kuwa katika Jumuiya moja na kuamini tupo salama kama hatutajifunza kwa wenzetu wanafanya nini katika mambo muhimu ya kiuchumi. Haiwezekani Uganda wakawa na kodi ndogo katika bidhaa za nguo wakati zinapita bandari za Tanzania au Kenya halafu sisi tukawa salama na viwanda vyetu vya nguo. Pia haiwezekanii DRC wakawa na kodi ndogo ya mafuta ilihali mafuta hayo yanapakuliwa Dar es Salaam, kama hatutafika katika uchumi wa kati.
Naomba niwasilishe kwa mawazo mbadala na mbinu za kukomboa janga hili