Tozi linanidondoka

Dam Boe

Senior Member
Jul 29, 2022
128
87
Naliandika kwa wino, tozi linanidondoka
Ni vipi hiki kibano, kwako nilichokikuta
Tozi linanidondoka.

Nilihisi nimefika, kwako nikajiburuta
Kiu yangu kadhalika, kubwa ilonikamata
Tozi linanidondoka

Ugeni ukaniponza, utakatifu kutaka
Mbio nilizozianza, nikazitoa sadaka
Tozi linanidondoka

Langu kubwa tumaini, wewe umelibananga
Ninaomba samahani,kwa yangu akili changa
Tozi linanidondoka

Ningejiweka rehani, usije inua tanga
Ili uwe furahani, ulize wangu nyakanga
Tozi linanidondoka

Nikupe ya kwetu pwani, unipe ya visiwani
Hila kwetu abadani, angeliafu manani
Tozi linanidondoka

Pigo ulilonichapa, limenitupa hewani
Mebaki natapatapa, wakumlilia nani
Tozi linanidondoka

Abadani asirani, mimi kwako sitamani
Namuepuka shetani, asinifanye jirani
Tozi linanidondoka
Swahibu Mlokole
Vikindu Pwani
23-10-2022.
 
Back
Top Bottom