TOYOTA RAV4 3 Doors For Sale - Dar es salaam. 6.7Mil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TOYOTA RAV4 3 Doors For Sale - Dar es salaam. 6.7Mil

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Ramthods, Jul 17, 2012.

 1. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wadau,

  Nauza RAV4 yangu kwenye picha hapo chini. Hii gari ni yangu mwenyewe, sio dalali.

  Mambo ya kufahamu ni kama ifuatavyo


  • Hii gari nilinunua mwaka 2009 toka kwa mdada ambae ndio original owner hapa bongo.
  • Ilikua imetembea ~97,000km, na sasa ipo 123,000km
  • Gari ilikua imported mwaka 2003 ikiwa na mileage 68,000km
  • Nimeitumia safari za mjini. Nimeshawahi kwenda nayo Bmoyo mara 3.
  • Engine sijawahi itengeneza, zaidi ya kubadilisha plug na oil kama service ya kawaida.

  Kwa atakae inunua, kuna matengenezo madogo kwenye body na kufanya kama ifuatavyo:


  • Vioo (cha dereva na abiria) vinapanda/kushuka slow sana. So utabidi ubadilishe machine.
  • Taa za mbele hazina mwanga vizuri (nadhan lens imechoka), na pia ya upande wa abiria imevunjika "lock". In short, taa za mbele ni za kubadilisha.
  • Ngao ya mbele imekatika kwa chini. So kama unavyoiona imelala kidogo upande wa dereva. Unaweza itoa, au ukanunua mpya au ukachomelea. Ni wewe utakavyojisikia.
  • Kwa upande wa mbele, nimebadilisha shock absorber zote, ball joint, na bush zote na makorokoro mengine. Ila shock absorber ya upande wa dereva ime "leak". Aliyeniuzia amegoma kunibadilishia, so ni ya kubadilisha.
  • Upande wa nyuma nimenunua shock absorber mpya, ila bush ni za kubadilisha, so zijazitoa bado.
  • Mlango wa nyuma unatoa sauti flani hivi ukipita kwenye mashimo. Huu mlango ulijigonga kwenye nguzo wakati gari inarudi nyuma. Ukiangalia kwa makini utaona kama umebonyea kiasi fulani hivi.
  • Kama utataka gari hii ipendeze, nunua seat cover.

  Hii gari alikua anatumia mama angu kwa muda, ila hapendi Auto, so nimemtafutia gari nyingine ya manual. Kwa sasa haina mtumiaji. Kama unadhani itakufaa, unakaribishwa.

  Zaidi ya mambo hayo hapo juu, hakuna matengenezo mengine nayojafahamu. A/C inafanya kazi kama kawaida. Radio inafanya kazi, ila inachagua sana CD.

  Nahitaji Tsh 6.7Mil. Wahi kabla sijabadili mawazo.

  Kama una maswali zaidi, ni PM.

  Karibu.

  UPDATE: SOLD OUT


  darshboard.jpg front.jpg front-right.jpg passenger-door.jpg radio.jpg reardoor.jpg rear-driver-side.jpg rear-side.jpg speedometer.jpg steering.jpg
   
 2. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wakuu,

  Hii gari ishapata mteja.
   
 3. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2014
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  long time sana hili tangazo
   
Loading...