TOYOTA IST Vs RAUM

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
289
Habari zenu wakuu.

Nimeamua kutumia mfano wa IST na RAUM katika hili swali langu ambalo kimsingi linajikita katika maswala ya Engine capacity na Vehicle weight.

Swali.
Je kuna utofauti wowote wa utumikaji wa mafuta au engine RPM kati ya magari mawili tofauti ambayo yanatumia engine zenye ukubwa sawa (cc 1500)....IST yenye cc 1500 ina uzito wa Kg 1030 lakini RAUM ina Kg 1150 kwa maana kwamba Raum ina Kg 120 zaid ya IST lakini zote mbili zinatumia same engine ambayo ni 1NZ Vvti.

Naendelea kuuliza....hii ina maanisha kuwa gari hiz mbili zikiendeshwa na watu wawil wenye uzito sawa....yaani IST dereva akawa na Kg 50 na Raum dereva akawa na Kg 50 basi engine mojawapo itakuwa imebeba mzigo zaidi ya nyingine na hivyo basi hata kwenye kuondoka kuna gari mojawapo itatumia rpm ya juu zaidi ili kutoa torque ya ku pull zile kilo ambazo zimezidi?

Nimejaribu kuandika kiurefu zaidi nia yangu ikiwa ni kueleweka ninachojaribu kuhoji hapa na kama kuna mtaalamu ambae ameelewa ni nin ninachokimaanisha naomba anisaidie kunielewesha zaidi inakuaje kuhusu matumiz ya hiz engine mbil je zitafanya kazi sawa au lazima kutakuwa na tofauti.
 
Mkuu kwanza hongera kwa mada nzuri, ni kweli fuel consumption inaendana na load ama mzigo gari uliyobeba. Capacity ya engine (CC)haipimwi kwa mzigo bali kiwango na displacement (jumla ya pistoni zote). Hivyo maximum amount of air displaced by the engine.

Unapoangalia uwezo wa mwendokasi ama vyote vinaweza kufikia kiwango kinachooofanana, hii inategemea mambo mengi

aina ya tairi, muundo wa body ya gari yenyewe, uzito uliyobebwa, driving habbit etc.

Kwa maana ya uwezo wa kustahili zinafana na utumiaji mafuta utategemea driving habbit.
 
Thanks
 
Back
Top Bottom