Top 10 ya majeshi hatari duniani kwa sasa na bajeti zake!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Jeshi ni sehemu muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa kiusalama.
Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake;

JAPAN-1.jpg


Wanajeshi wa Japani.

10: JAPAN
Japan ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia (WW2) iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo, Japan iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la kawaida lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua tena jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake.

Bajeti ya Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 49.

Jeshi hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000 waliopo kazini na zaidi 60,000 wa akiba. Lina ndege za kivita zipatazo 1,595 na meli 131.

KOREA-KUSINI.jpg


Wanajeshi wa Korea Kusini wakifanya mazoezi.

9: KOREA KUSINI
Korea Kusini wanashirikiana mpaka na Korea Kaskazini ambao nao wapo vizuri kijeshi. Ili kukabiliana na majeshi makubwa ya China and Japan, Korea Kusini imekuwa ikiongeza bajeti ya jeshi lake hadi kufikia dola bilioni 34.

Lina wanajeshi waliopo kazini 640,000 na wengine wa akiba 2,900,000. Lina ndege kubwa za kivita 1,393 na meli za kijeshi 166.

UTURIKI.jpg


Wanajeshi wa Uturuki.


8: UTURUKI
Labda ni kwa sababu ya kushirikiana kupambana na kundi korofi la kigaidi la Islamic State linalotishia amani duniani ndiyo maana ni kubwa na linaogopeka zaidi. Limeongeza bajeti yake kwa 10% hadi kufikia dola bilioni 18.

Lina wanajeshi wapatao 660,000 walioko kazini na wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na silaha za nchi kavu 16,000 likiwa lina ushirikiano mkubwa na lile la Marekani.

UJERUMANI.jpg

Wanajeshi wa Ujerumani.

7: UJERUMANI
Miongoni mwa nchi zenye majeshi hatari duniani ni Ujerumani. Linatengewa bajeti ya dola bilioni 45, japokuwa linaonekana kushuka katika miaka ya hivi karibuni labda kwa sababu kizazi cha sasa nchini humo hakipendi mambo ya vita na watu wengi wanaogopa kujiunga na jeshi hilo.

Lina wanajeshi 183,000 walioko kazini na 145,000 wa akiba likiwa na ndege za kivita 710 na silaha za nchi kavu zaidi ya 5,000.

UFARANSA.jpg


Wanajeshi wa Ufaransa.


6: UFARANSA
Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imepunguza bajeti ya jeshi lake hilo kwa 10%. Bajeti yake inafikia dola bilioni 43 kwa mwaka. Lina wanajeshi 220,000 waliopo kazini na 500,000 wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na vifaa vya nchi kavu 9,000.

UINGEREZA.jpg


Waajeshi wa Uingereza.


5: UINGEREZA
Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao wapo kwenye mkakata wa kupunguza wanajeshi wake kwa 20%.
Bajeti ya jeshi lake hatari ni dola bilioni 54 kwa mwaka likiwa na wanajeshi 205,000, ndege za kivita 908 na meli 66.

INDIA.jpg


Wanajeshi wa India wakiwa katika mazoezi.


4: INDIA
Jeshi lake lina jumla ya ‘wajeda’ milioni 3.5, wakiwemo milioni 1.325 waliopo kazini na wengine ni wa akiba. Lina magari ya kivita 16,000 na ndege 1,785 pamoja na silaha za nyuklia. Bajeti yake ni dola bilioni 46.


Wanajeshi wa China.

3: CHINA
Bajeti ya Jeshi la China inafikia dola bilioni 126 likiwa na wanajeshi milioni 2.285 waliopo kazini na milioni 2.3 wa akiba. Ni moja ya majeshi makubwa kwa sasa duniani likiwa katika Tatu Bora.
Lina vifaa vya kivita vya nchi kavu 25,000 na ndege 2,800. Pia lina silaha za nyuklia 300.

URUSI.jpg


Wanajeshi wa Urusi.


2: URUSI
Bajeti ya jeshi hatari la Urusi ni dola bilioni 76.6 ambayo inatarajiwa kuongezwa kwa 44%.
Tangu alipoichukua Urusi, Rais Vladimir Putin mwaka 2000, nchi hiyo imekuwa moto wa kuotea mbali katika masuala ya kijeshi. Lina wanajeshi 766,000 waliopo kazini na milioni 2.5 wa akiba. Urusi inaongoza kwa silaha za kivita zikiwemo za nyuklia zipatazo 8,500.

MAREKANI.jpg

Wanajeshi wa Marekani.

1: MAREKANI
Jeshi kinara la Marekani linatengewa bajeti ya dola bilioni 612.5. Hakuna jeshi lenye bajeti kama hiyo duniani. Lina wanajeshi milioni 1.4 waliopo kazini na 800,000 wa akiba. Hawa jamaa ni wabaya kwa ndege, meli na manowari za kivita. Pia lina silaha za nyuklia 7,500. Kama ulikuwa hujui ndilo jeshi namba moja duniani tangu Vita ya Pili ya Dunia iliyomalizika mwaka 1945.
Nchi kama Urusi na China zinangoja sana kwa jeshi la Marekani kutokana na kuwa na mbinu na teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi.

NB: Data kama hizi ni vigumu kuzipata kwa baadhi ya nchi za Afrika.
Imeandaliwa na Sifael Paul kwa msaada wa mtandao.

Top 10 ya majeshi hatari duniani kwa sasa na bajeti zake!
 
Niliangalia mwaka jana budget yao ni kubwa sana kwenye jeshi hata idadi yao iko juu
 
Iyo orodha sio,saudi arabia kwa bajeti ya kijeshi inashika nafasi ya nne,baada ya marekani,russia na china.
Hata kwa vifaa inavyo vingi na inasemwa saud arabia airforce inaiovertake hasa israel
 
Kama issue ni bajeti na idadi ya wanajeshi ok. Ila kama ni mbinu kali, kujituma, n.k. something is wrong. Where is IDF?
Ni kweli kwa vigezo vya kujituma, mbinu na uzalendo nafkri Tanzania tunaweza kuwepo kwenye top 10 na Urusi ni no. 1
 
hapo ukijumlisha wote utapata
marekani,china na urusi, wengine wote ni vibaraka wa marekani(pamoja na budget yao hawawezi hata kumbishia).
Hiyo hali ya kutegemea marekali ni kigezo tosha cha kuweka hayo majeshi dhaifu ulimwenguni. Alafu hao vibaraka wa marekani pamoja na marekani yenyewe wanajeshi wake wanaogopa kufa balaa, sasa kwa hali hyo kuna uimara kweli?
 
Back
Top Bottom