Toka Bungeni: Nyumba 4,036 kujengwa kwa ajili ya askari Polisi, kupata mkopo kutoka Benki Exim China

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali imepanga kujenga nyumba 4,036 ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba za wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya ndani

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Momba Mkoani Mbeya David Silinde (CHADEMA) aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutatua kero kuu ya askari polisi kukosa nyumba za kuishi pamoja na ofisi za kufanyia kazi.

''Mheshimiwa Spika Serikali inatambua uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani hasa askari polisi.

"Ili kutatua tatizo hilo tumejipanga kupata mkopo kutoka benki ya Exim China ili kujenga nyumba 4,036 za polisi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa zaidi nchini''. Amesisitiza Masauni.

Aidha Serikali imesema nyumba hizo zitahusisha pia upande wa Unguja na Pemba katika mgawanyo utakao kwenda kwa awamu mbalimbali.
 
Halafu mtazirudishaje hizo pesa?? Kwanini wasitumie kitengo chao cha ujenzi na cha magereza kufyatua tofali na kujenga
 
  • Thanks
Reactions: nao
Hiyo tenda kwa nini wasipewe JWTZ, maana wakishirikiana na JKT pesa nyingi itaokolewa, isitoshe tutatumia pesa yetu ya ndani, au JWTZ hawatoi 10%?.
 
Serikali imepanga kujenga nyumba 4,036 ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba za wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya ndani

Hizi ndizo habari wananchi wanataka kusikia sio za yule mbunge wa Chadema ubungo SAID KUBENEA aliyeongelea mambo ya kuvuliwa chupi na shanga.Heko mawaziri wa CCM
 
Hiyo tenda kwa nini wasipewe JWTZ, maana wakishirikiana na JKT pesa nyingi itaokolewa, isitoshe tutatumia pesa yetu ya ndani, au JWTZ hawatoi 10%?.

Naona umeenda mbali.Hawajafikia utoaji tenda bado.Kinachoongelewa hapo ni mkopo.Ukishapatikana tenda zitaitishwa atakayeshinda atapewa kama ni mchina au mtanzania au JWTZ au JKT.Vuta subira hadi wakati huo wa tenda ukifika.
 
Serikali iache huu upuuzi na akili za matope wa kujengea nyumba watumishi, hao polisi wakapange au wakakope wajenge nyumba zao kama watumishi wengine
 
Hizi ndizo habari wananchi wanataka kusikia sio za yule mbunge wa Chadema ubungo SAID KUBENEA aliyeongelea mambo ya kuvuliwa chupi na shanga.Heko mawaziri wa CCM
Bahati yako hakuna kile kitufe cha kukupa dislike maana ningekupatia 1000,0000 dislikes, akili zenu ka kina Makonda eti walimu wasilipe nauli then leo polisi nao wajengewe nyumba huu ukurupukaji utaisha lini
 
Back
Top Bottom