1.Mvulana atatembea na msichana bila kinga,halafu akiletewa taarifa ya mimba,ataruka
na kukimbia....Mwanaume atajadili na huyo msichana nini kifanyike.....
2.Atamuacha mkewe ambae hana kazi wala biashara bila matumizi ya kutosha..
halafu ataanzisha ugomvi mkubwa akihisi mkewe 'anatoka nje'....Mwanaume atapigania
mahitaji ya mkewe na watoto kwanza kabla ya kuanza 'kuunguruma'nyumbani..
3.Mvulana akipata mshahara moja kwa moja bar na atarudi nyumbani kesho yake....
Mwanaume ataingia bar pale anapoona hali inaruhusu tu...
4.Mvulana atashangaa 'kudondokewa na kuzimikiwa na mwanamke'
Mwanaume hushangaa kumtongoza mwanamke na 'kumkosa'
5.Mvulana akimnunulia bia mwanamke lazima 'alipwe'
Mwanaume huwa hadai 'malipo' kwa kumpa bia au favour mwanamke
but anaweza tu kukataa akiona sio lazima..
6.Mwanaume hujali zaidi 'heshima' yake....
Mvulana hujali zaidi 'tamaa' yake....
7.Mvulana hupiga kelele au kuguna guna au kutoa sauti au kubadilika tabia
akiona 'mrembo ' kaingia au anapita karibu...
Mwanaume hujifanya hajaona kitu,sana sana akiamua 'huchukua hatua'
muafaka....kimya kimya...
8.M wanaume hukubali kukosa kama gharama za kupata ni kubwa mno...
Mvulana hung'ang'ania 'apate' hata kama gharama 'zitamuumiza' ...
9. Mwanaume huwa 'anajifunza 'kila siku
Mvulana huamini 'anajua' yote...
10. Mwanaume hufikiria maisha kwa ujumla na 'future' ya watoto...
Mvulana anafikiria pamba,magari,warembo 24/7......
Mengine mnaweza kuongezea.......wanasema kuna 'mvulana' kwa kila mwanaume
but wengine huwa wanabaki kuwa 'wavulana' milele.........lol......
ANGALIZO= HAPA NAZUNGUMZIA WATU MNAOFAHAMIANA TAYARI SIO ONLINE PEOPLE AMBAO HUJAKUTANA NAO
NA UANZE KU WA JUDGE KWA POST TU ZA HUMU...