Tofauti ya ubongo wa mwanamke na wa mwanaume

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,934
1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume hawezi.

2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.

3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo huo ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso. Guys, next time ukiwa unamdanganya msichana ni better mkiwa hamko uso kwa uso.

4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbali na kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.

5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.

6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.
 
umeongelea manyoya tu, nyama umeacha, gegedo?!!
 
Akili Unazo! YOUR THREAD IS CONTRARY TO YOUR SIGNATURE...WEIRD...

What does my signature say??? What does your signature say? Do you think always as your signature say?.Sioni mahusiano ya thread na signature ya mtu. Asante kwa mchango na angalizo.
 
What does my signature say???
To every successful man, there is a very complicated woman who is causing a headache behind!. Bobi Wine
What does your signature say?
THE TWO ENEMIES OF HUMAN HAPPINESS IS PAIN AND BOREDOM.
Do you think always as your signature say?
evidently
Sioni mahusiano ya thread na signature ya mtu.
paradoxical

Asante kwa mchango na angalizo.
thank you
 
tuanzie hapa,ubongo ni nini?

Ahaa ubongo ni kiungo cha muhimu kinachopatikana ktk vichwa vya viumbe hai kasoro mimea, ila ingawa ni wa muhimu waweza kubeba aidha akili au matope, achante mwaliaalim.
 
1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV. Mwanaume hawezi.

2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.

3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo huo ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso. Guys, next time ukiwa unamdanganya msichana ni better mkiwa hamko uso kwa uso.

4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbali na kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.

5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.

6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.

Upo right mkuu ningefurahi zaidi kama ningeumbwa na ubongo wenye sifa hizo lkn mwili na viungo vyake ubaki huu huu wa kiume...
 
Kwa hiyo unataka kusemaje? yaani "conclusion" yako ni nini baada ya kuelezea hizo tofauti za ubongo wa mwanaume na mwanamke?
 
Mada kama hii hunifanya nizidi kuustajabia uumbaji wa Mungu kwa jinsi ya tofauti,ubarikiwe ndugu mleta mada kiukweli umeniongezea maarifa ya kucope na Mke wangu kipenzi,raaaaha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom