Barakaeli174
Senior Member
- Aug 2, 2015
- 171
- 142
Wana JF,
Naomba kwanza niulize, kwanini Waziri kama ambaye ni msomi na sio darasa la 7, amejitoa akili kukubaliana na hoja na kutangaza kuwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya hupewa vyeo hata kama hawajui kusoma na kuandika na vyeti vyao haviwezi kukaguliwa.
Sasa hekima ipi tutegemee kwa watu kama hawa wanao ongoza eneo kubwa lenye watu wasomi na wasio wasomi, kwa mtazamo wangu madhara yake yaweza kuwa kama ifuatavyo:
1. Kwa mtazamo wangu haya yatakuwa na madhara makubwa sana katika nchi hii na si ajabu madhara mengi na matatizo mengi tunayoishimo si ajabu yanatokana na maamuzi kama haya ila hatujajua tu kuwa matatizo haya yanatokana na nini sasa tumeanza kufunguka kuelewa mengi; matamshi hayo ya mamlaka teuzi wanatoa picha kuwa hata wao elimu yao lazima ichunguzwe kabisa tena bila shaka, uwezo wao wa kufikiria ni mdogo sana, wanakichafua chama chao kuwa maamuzi ya chama ni ya hovyo, wanadhihirisha kuwa chama kina watu wasio na uwezo wa kuwaongoza watanzania na watakuwa wanaongoza sio kwa uwezo bali kusaidiwa na nguvu za dola maama wanapofikiria wanajua kumbe hawajui, wanahitaji msaada mkubwa sana kabla ya kufanya maamuzi.
2. Haya maamuzi yatawasumbua sana wananchi na kujikuta kusimamiwa na watu ambao watakuwa ni tatizo na sio watatuzi wa matatizo, Wananchi wanajiona wanaongozwa na watu wenye mihemuko, wananchi wana wasiwasi kuwa wataishi kwa kuteswa na kutendewa mabaya kwakuwa wana viongozi wasio na uwezo wa kuelewa kile wanachokifanya kuwa kina madhara kisiasa kiuchumi na kifedha wao wanaamua na ndivyo ilivyo, mfano mtu anaamua kufunga kiwanda na kukipa masharti magumu au kuongeza kodi bila ya kujua kuwa kiwanda hicho kina madhara makubwa kwanza ajira zitapotea, serikali itapoteza mapato yake kwa kipindi hicho na mwenye kiwanda atapata hasara maana uwekezaji wake unahitaji fedha za kurudisha mtaji...sasa huo uongozi unaoamua kufunga kiwanda una uwezo wa kufikiria kweli kuna njia mbadala ambao hauwezi kuathiri vyote tajwa. Unaamua kumnyanyasa muwekezaji na kuingilia mali yake je akihamisha na kufunga biashara zake kwa mihemuko yako je wale walio ajiriwa utawapeleka wapi najua huna, familia zao utazilea huwezi kwa hiyo kuna njia mbadala ambayo unaweza ukamshtaki kwa kukiuka sheria za nchi bila ya kuathiri uwekezaji wake.
3. Mkoa au wilaya haitaongozwa kwa kiwango kinachotakiwa, kwa sababu uongozi wa mkoa au wilaya unaongozwa na mtu asiye na uelewa wa kujua aisaidie nchi vipi ili iwe ya viwanda na yenye uchumi wa kati kwa kuanzia katika eneo lake na haita wahi kutokea, huyu kiongozi ndiye aliyepo chini kuangalia mazingira na hali ya ardhi na kutoa rathmini ya eneo husika la kwake kuwa kipi kifanyike katika eneo lake ili wapate nini.
Sasa wana JF, hili lina shangaza sana, mataifa lazima wacheke sana na hii aibu hatujui pa kuipeleka, katika ajira serikalini inaonesha kuwa asiye na cheti chochote bali anayejua kusoma na kuandika tu ataishi kwa mshahara wa zaidi ya sh 6,000,000 na aliye na degree hata masters ataishi kwa mshahara wa sh 800,000 au chini ya hapo, waalimu na madaktari wazidiwe mshahara na aliyejua kusoma na kuandika tu hajaenda darasani hivi kweli. Ndio maana mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wana wafukuza kazi na kuwatukana na kuwasema vibaya watumishi hawa kwanza ni kwa sababu wanajua wanawazidi mishahara pia wana elimu ndogo kuliko wao walio wasomi na hawawezi kuwafanya lolote.
Kuna hatari ya kuleta kitu ambacho hakijawahi fika hapa tanzania na kufanyika.