Tofauti ya Lowassa na Magufuli hii hapa

Tofauti ya Lowassa na Magufuli hii hapa

romaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
477
Reaction score
218
Habari wakuu

Hii nimeipata mahali nikaona vema kushare hapa

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.

Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k.

Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi.

Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Mtu huyu ni Edward Lowassa.

Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa. Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara. Tuangalie mifano:

Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!
Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli
amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA.
Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA.
Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA. Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.
Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumziko ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA.

UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA.
 
Take all my 'likes'....
Lowassa... a true presidency material!!

Nyie watoto, beba madeli yenu mkauze maji.Lowasa hawezi kushnda.Hıı haijapote kiasi cha kukabidhi nchi kwa wendawazimu na walanguzi.HATASHNDA, USIPOTEZE MUDA NA JASHO LAKO KUMTETEA.
 
romak

Hizi ndio nondo tunazozitaka, imetulia sana mkuu. sio maccm yanakuja na hoja ya ufisadi kwa kumtuhumu Lowasa wanaambiwa leteni ushahidi au nendeni mahakamani. matokeo yake wamebakia na majungu na zilipendwa.
 
Last edited by a moderator:
Nyie watoto, beba madeli yenu mkauze maji.Lowasa hawezi kushnda.Hıı haijapote kiasi cha kukabidhi nchi kwa wendawazimu na walanguzi.HATASHNDA, USIPOTEZE MUDA NA JASHO LAKO KUMTETEA.

Mkuu toa hoja kwanini atashinda..??? sio unaleta majungu na kujifariji wakati mwenyekit wenu le profeseriii anataka kukimbia nchi.
 
Nini dhamira ya kutangaza nia?Kitendo cha kuchukua ndo kutangaza nia kwenyewe.Kp nipo HP, ningeshndanishwa na Lowasa, ningemshnda kiushawishi na kujenga hoja.Jamaa lenu halijiwezi jamani.
 
kwa nini sasa lowassa hakujiuzuru mapema kulinda heshima yake kama alikuwa na mashaka na mkataba ule?
 
Hakuna unalolijua rudi darasani kasome nyayo za mkapa alipataje urais kabla ya kikwete. Macho yanakutoka, mishipa imekusimama hoja huna umekalia ushabiki tuu. Wapiga kura wapo kijijini sio nyinyi vibaka wa mjini. Buku 10 za mafuta ya bodaboda ili mjaze front pages.
 
Nyie watoto, beba madeli yenu mkauze maji.Lowasa hawezi kushnda.Hıı haijapote kiasi cha kukabidhi nchi kwa wendawazimu na walanguzi.HATASHNDA, USIPOTEZE MUDA NA JASHO LAKO KUMTETEA.

We ndugu yangu mbona ka ndo unatapatapa? Mimi nasema lowasa atashinda kwa sababu tutampigia kura wewe unasema hatashinda kwa kutegemea goli na mkono au?
 
Hizi ndio nondo tunazozitaka, imetulia sana mkuu. sio maccm yanakuja na hoja ya ufisadi kwa kumtuhumu Lowasa wanaambiwa leteni ushahidi au nendeni mahakamani. matokeo yake wamebakia na majungu na zilipendwa.
ndo madudu gan hayo Kwan Lowasa yeye hana negative
 
Magufuli ndiye raisi wa Tanzania, full stooop....hayo mengine ya lowasa mnajifariji tu.....kibaka hawezi kupewa ikulu kamwe
 
Magufuli ndiye raisi wa Tanzania, full stooop....hayo mengine ya lowasa mnajifariji tu.....kibaka hawezi kupewa ikulu kamwe

Toa hoja kwamba kwanini lowasa hafai kuwa raisi pia dhibitisha huo ukibaka wake
 
Back
Top Bottom