Tofauti ya kufikiri na kuwaza

Tofauti ya kufikiri na kuwaza

mypmuh

Member
Joined
Nov 15, 2014
Posts
18
Reaction score
23
Kuna jambo moja ambalo watu hushindwa kutofautisha.
1) Kuwaza
2) Kufikiri

Kwa kuyatazama mtu anaweza dhani ni kitu kimoja lakini katika uhalisia ni vitu viwili tofauti na 95% huwaza ila 5% ndio hufikiri. Mawazo kila binadamu anayo ila Kufikiri ni watu wachache tu ndio wamebahatika kuingia kwenye kundi hili. Unaweza Kuwaza namna unavyoweza kumiliki chombo cha usafiri ila mwingine akafikiria mbinu za kupata hicho chombo na namna kitakavyoweza kumsaidia na akatengeneza mpango kazi.

Kwa siku binadamu anaweza kupata Mawazo zaidi ya milioni lakini kiuhalisia kwa siku mtu asifikirie kitu. Watu wengi ni wazuri sana kwenye kuwaza ila wengi ni wabovu kwenye kufikiria na ndipo mmiliki wa kiwanda cha magari Henry Ford aliposema "kufikiria ni kitu kigumu sana ndio maana watu wachache sana hufikiria" wengi hujidanganya kwa elimu zao na kudhani walicho nacho kichwani ni fikra kumbe ni Mawazo, tofautisha kati ya moshi na moto...wengi huishia kwenye moshi na sio kwenye moto.

Wanaofanikiwa wengi hufikiria na sio kuwaza. Nenda Bar kutana na walevi au vijiweni kutana na vijana utashangaa wana Mawazo mazuri sana lakini sio kwamba wana fikra nzuri sana. Fanyia kazi hili nawe utajiona tofauti kabisa. acha kuwaza na anza kufikiria. Unawaza kujenga ghorofa lakini hufikirii kujenga ghorofa. Niwatakie jioni njema wapendwa.
 
Kuna jambo moja ambalo watu hushindwa kutofautisha
1) Kuwaza
2) Kufikiri
Kwa kuyatazama mtu anaweza dhani ni kitu kimoja lakini katika uhalisia
ni vitu viwili tofauti na 95% huwaza ila 5% ndio hufikiri.
Mawazo kila binadamu anayo ila Kufikiri ni watu wachache tu ndio
wamebahatika kuingia kwenye kundi hili.
Unaweza Kuwaza namna unavyoweza kumiliki chombo cha usafiri ila
mwingine akafikiria mbinu za kupata hicho chombo na namna
kitakavyoweza kumsaidia na akatengeneza mpango kazi.
Kwa siku binadamu anaweza kupata Mawazo zaidi ya milioni lakini
kiuhalisia kwa siku mtu asifikirie kitu. Watu wengi ni wazuri sana
kwenye Kuwaza ila wengi ni wabovu kwenye kufikiria na ndipo mmiliki
wa kiwanda cha magari Henry Ford aliposema "kufikiria ni kitu kigumu
sana ndio maana watu wachache sana hufikiria"
Wengi hujidanganya kwa elimu zao na kudhani walicho nacho kichwani
ni fikra kumbe ni Mawazo, tofautisha kati ya moshi na moto...wengi
huishia kwenye moshi na sio kwenye moto.
Wanaofanikiwa wengi hufikiria na sio Kuwaza. Nenda Bar kutana na
walevi au vijiweni kutana na vijana utashangaa wana Mawazo mazuri
sana lakini sio kwamba wana fikra nzuri sana.
Fanyia kazi hili nawe utajiona tofauti kabisa. Acha Kuwaza na anza
kufikiria.
Unawaza kujenga ghorofa lakini hufikirii kujenga ghorofa.
Niwatakie jioni njema wapendwa.
Copy and paste
 
Thus why wagunduzi wa vitu ni wachache, unachukua muda mtu kufikiria jambo na hatimaye kuja na ufumbuzi
 
Back
Top Bottom