Tofauti ya Dira ya Taifa na ilani za vyama

Tofauti ya Dira ya Taifa na ilani za vyama

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Leo nimekuwa nikisoma Ilani ya CCM kuangalia masuala mbalimbali waliyoeleza kwenye sera yao kwenye harakati zao za kuomba ridhaa kuendelea kuongoza.

Theoretically, Ilani ya Chama inabidi kuelezea namna inaenda kuielekea Dira ya maendeleo ya Taifa. Lakini badala ya kuona namna ambavyo ilani inaelezea namna ya kuitekeleza dira ya taifa naona iko na vitu ambavyo havina tofauti na dira. Yaani Ilani na zenyewe ni kama Dira. Ilani Comprehensive ya CCM ina sura tano, wakianza kuelezea mafanikio kisha kuanza kuweka ahadi.

Suala hili sio wao peke yao, hata vyama vingine viko hivyo. Sasa ilani inapokuwa sawa na dira ya taifa inaondoa maana ya demokrasia, maana mtu unachagua kitu gani? Kama CCM anaahidi hospitali, hata ACT anaahidi hospitali, hapa hauna chaguo.

Kinachotakiwa kuchaguliwa ni kwa namna gani tunapata hospitali, ambapo ilibidi tuone mmoja labda anasema tutajenga kwa nguvu za wananchi, mwingine anasema tutakopa nje, mwingine akasema tutawatoza kodi wafanya biashara ili tupate ya kujenga hospital. Hapo mwananchi anapima hiyo njia kuona inamuumiza kiasi gani ili akichagua anachagua njia ambayo anaona iko rafiki kwake.

Sielewi siasa zetu zinazingatia nini kwenye kutengeneza mikakati ya kampeni, maana nasikia ahadi tu zisizo na mkakati, ambazo ahadi hizo ni sawa na dira ya taifa. Mathalani Dira inalenga kuwa na ajira kiasi kadhaa kufikia 2050, chama inabidi kituambia kitafanya nini kutimiza lengo hilo la dira, ila chama kikisema kitatengeneza ajira hapa inakuwa ni duplication ya kilichosemwa na dira.

Umri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom