Wakuu habar za jioni,
Poleni na majukumu ya kutafuta pesa,"tujadili haya maneno 2 MAPENZI na UPENDO
Nijambo ninalojiuliza kwa mda kidogo tofauti ya MAPENZI na UPENDO
MAPENZI ni matamanio ya mwili, tendo la kufanya mapenzi, mnaweza mkawa na mapenzi bila upendo, watu wengi wanaangaika na MAPENZI hawapo kwenye upendo.
Mfano: Mwanaume anamuangalia mwanamke na kutamani kufanya nae MAPENZI tu, ena akimuona mwanamke mwenye makalio makubwa, mguu wa bia au mwanamke chuchu saa 6 na kadha wa kadha hapo ni mapenzi ndio yanamsukuma hakuna UPENDO.
Mwanamke ametawaliwa na mapenzi anasema namtaka mwanaume mwenye 'six packs', gari zuri, mrefu and so so hapo ni mapenzi yametawala hakuna UPENDO.
Kuna watu wengi hawajawahi KUPENDANA ni MAPENZI tu ndio yamewaunganisha, MAPENZI ni tendo na tamaa ya mwili,J E mapenzi yakiisha kitaendelea nini?
MWANAMKE
Ndio maana ukijua leo unaenda kukutana na mtu wako unakamia sana unaangaika sana, utajipamba haswa hata kama huna pesa ya salon utakopa ili upendeze. Utaweka vitu sehemu za siri ili ukamnogeshe jamaa hapo hakuna UPENDO hayo ni mapenzi, kwenye upendo hakuna mbwembwe.
MWANAUME
Akijua anaenda kukutana na mtu wake anakamia haswa mara anywe supu ya pweza,mara udongo wa congo,atumie dawa za kuongeza uume au nguvu za ume hapo hakuna UPENDO unawaza mapenzi tu.
Tunatumia nguvu kubwa kutengeneza MAPENZI tunakosea sana inabidi tutumie nguvu na akili zetu zote kujenga UPENDO.
UPENDO
Kwenye UPENDO kunabaraka nyingi sana, kwenye upendo hakuitaji mpaka utumie vumbi la Kongo kwani mambo yatajiseti yenyewe. Kwenye UPENDO unajenga urafiki ambao hamta ogopana, mtaongea, mtacheka, mtafurahi na kila kitu kitakuwa sawa.
Kwenye upendo hakuna kukashifiana mara oooh huyu anakibamia au huyu anarambo au unamuona mwenzio mbwa,au unamuna kama mwanaume mwenzio au mwanamke mwenzio.
Jiulize uko kwenye MAPENZI au UPENDO.
Nawatakia Jioni njema. Povu ruksa.
Mapenzi ya kweli na upendo vyote ni attribute za Mwenyezi Mungu. Huwezi KAMWE kusema unapenda kama hujajaliwa na Mungu, utakuwa unafuata mkumbo tu. Why?
Biblia inasema pendo latoka kwa Mungu, Yeye alitupenda KWANZA kabla sisi hatuja mpenda wala kumjua. Sasa mfano wetu wa kupenda ni jinsi alivyotupenda ingawa tu wadhambi. Hii ina maana gani?
Ukiingia kwenye ndoa, fahamu kuwa UPENDO hujengwa, mwanamume ndio mwenye wajibu wa kujenga upendo. Sasa kama ndivyo, mwanamke HUJAPEWA KUPENDA hata kidogo, ni kujitwika jukumu lisilo lako. Mungu amelipensa kanisa, lakini anategemea UTII kutoka kwake. Upendo ni one way taraffic, kutoka juu Mungu analipenda kanisa, ndani ya kanisa nako mume anampenda mke, halafu mke anamtii mume kama jinsi kanisa linavyomtii Mungu.
Ukienda kwa mtindo huo moyo wa mwanamume utaumiliki, kwani utii una nguvu kubwa mno kuliko upendo. Mwanamume hupumbazwa na utii akafumbwa macho na kujiona mwenye bahati ya kuoa MALAIKA kati ya wanadamu. Lakini kama mke atakesha mitandaoni akilalamikia upendo kama yeye ANAVYOMOENDA MUME, basi aelewe kuwa amekiuka msingi wa ndoa na kinachofuata vinjemba vya pembeni vitamzuga kwa upendo wa mshumaa ili vimtumie hovyo. Hivyo ndivyo roho ya uzinzi inavyoingia ndani ya familia na watu kuchukiana kwa sababu ya kuzini hovyo.
Ushauri wa bure, roho ya uzinzi msiikaribishe ndani ya nyumba yenu hata mara moja. Kama ukiona kuna jambo limepungua, njia nyepesi kabisa ya kumrejwza mwanamume ni kujishusha kwa kudhamiria na kuwa kama mjinga. Mwanamume yeyote ambaye ni mume akiona hivi lazima ataguswa moyoni mwake badala yake yeye ndiye atakayeomba amani ndani ya nyumba na furaha itarejea tena.
NI DHAMBI KUBWA MWANAMKE KUSHUPAZA SHINGO ndani ya ndoa, matokeo yake ni kuishi kwa kuvumiliana jambo ambalo mwishowe ni kutalikiana. Usiujaze moyo wa mwanamume masimango na maneno ya kuumiza kwa kudhani unamkomoa, mara zote mwanamke mwema ni mwenye maneno machache mno, tena akiongea hata kama mwanamume atakuwa amefura hasira vipi, baadaye akikaa hujitafakari na kujutia kauli zake. Lakini mwanamke mpambanaji hujipalia makaa juu ya kichwa chake mwenyewe.
Neno moja tu: KAMA UPENDO WENYE WATOKA KWA MUNGU, BASI HAKUNA MTU WA KATI ATAKAYEWEZA KUWAINGILIA NA KUWAVURUGA HATA KAMA UMEPISHANA VIPI, KWANI HOFU YA MUNGU ITAKUWA NDANI YA MIOYO YENU DAIMA.
Mwanamke ametawaliwa na mapenzi anasema namtaka mwanaume mwenye 'six packs', gari zuri, mrefu and so so hapo ni mapenzi yametawala hakuna UPENDO.
Kuna watu wengi hawajawahi KUPENDANA ni MAPENZI tu ndio yamewaunganisha, MAPENZI ni tendo na tamaa ya mwili,J E mapenzi yakiisha kitaendelea nini?
Kama umeingia kwenye ndoa kwa mtazamo huo, basi wewe hukustahili kuolewa kwani hakuna hata sifa moja ya ndoa katika hayo. Six park ni mambo ya nje ya mwili tu, ni mambo yanakuja na kupita. Gari nzuri ni ipi? Urefu ni nini? Katika hayo hakuna mapenzi bali ni upofu na kujilisha upepo.
Unataka mapenzi ya kweli? Basi tafuta kweli ya mapenzi kwanza. Ndani ya ndoa mambo hubadilika kadri siku zinavyokwenda, sasa ,wombe sana Mungu awajalie mambo yenu yawe mazuri tu daima. Ikitokea mkwamo kidogo lazima utatoka nje ya ndoa kwa sababu hukuwa tayari kwa ndoa. Ni vema basi kujifunza misingi ya ndoa kabla ya kuingia kweny ndoa.
Nina mfano wa kweli kabisa wa jamaa yangu ambaye aliingia kwenye mgogoro mdogo tu na mkewe, mwanamke aliamua kutafuta liwazo nje na kila mara alionekana maeneo ya Mara Courtyard Motel akipumzishwa. Mara hiyo mume akawa si lolote, hana jipya wala haana mvuto wa mapenzi.
Sasa kwa mitazamo ya wanawake wengi, kukorofishana na mume ni tiketi ya kufanya uzinzi. Kwa wanawake na wanaume wote wenye mitazamo ya namna hii, eleweni kuwa hamna Mungu ndani yenu, ninyi mnaigiza tu. Imewapasa kufanya tiba ya kweli na Mungu ji mwenye rehema atawarejeza kwani upendo wa kweli unatoka kwake tu.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
View attachment 1325414