Mkuu umetoa maelezo mengi bila kuhitimisha unalenga nini? Licha ya pale ulipoandika kuna tofauti kati ya liability na asset.
Labda kwa kujazia , nafikiri unataka kumaanisha kwa nini watu wanakuwa maskini na wengine wanakuwa matajiri.
Moja wapo ni kuweza kujua kanuni za kifedha au ujuzi wa kifedha ( financial intelligence).
Wakati maskini na mtu kati ( middle class ) analimbikiza liability ( mfano nyumba ya kuishi, TV inch 55 na kuendelea, magari ya anasa na vingi kama hivyo), upande mwingine kuna yule anamiliki asset ( vitu ambavyo vinaleta mapato ) anafungua biashara, anajenga nyumba ya biashara, ananunua viwanja nk nk.
Hivyo anaendelea kukusanya really asset anakuwa tajiri. Yule anayekusanya liabilities akifikri anamiliki asset, mwishowe huwa anajikuta yupo hohehahe...