Tochi za barabarani sasa faini 200,000. Tanroads wasema faini hiyo ni halali ipo kisheria

Acheni uzushi mbweha nyie. Mimi baada ya kuona hapa, nimeenda kukanyaga mpaka 120 nikapigishwa faini ya 30,000 nikawauliza mbona wamechaji kosa moja tu, wakaniambie niachane na habari za vijiweni kwani hakuna faini ya aina hiyo duniani. Ukiharibu au kutishia kuharibu miundo mbinu ya barabara hapo ndiyo hukunyuka TANROADS faini
Inaleta mantiki pale unapoharibu miundombinu.labda huyo alioverspeed na kuoverload
 
Ni matumizi mabaya ya sheria.
Sheria zote inapotokea kuingiliana katika adhabu kwenye kosa moja ambalo linafanana basi sheria hizo hutamka kuwa adhabu itakayo tumika zinazohusiana na kosa hili zitaamuliwa na sheria fulani.
Mfano kosa la speeding kama limetajwa kwenye sheria za Tanroads
Sumatra
Na Road Trafic Act basi adhabu itatolewa na sheria moja tu katika hizo .
Kunakuwa na default sheria itayotumika na sio kutoa adhabu ya kosa moja kwa kila sheria
Haya ni matumizi mabaya ya tafsi ya sheria. Lengokuu ni kukomoa hasa hasa baada ya kuona kodi au faini itokanayo na faini za barabarani zime pungua sana kutokana na madereva kuwa waangalifu sana siku hizi

Pia kuna tatizo la kukomoana sana kwenye speeding ..nchi nyingi zinatoa allowance fulani katika kosa hili kwani kuna kuna tatizo la kupunguza speed unapo ingia eneo la speed limit.
UAE wana allow 20kms
Europe 10%
US na Canada 15%
Sisi kwanza Kuna tofauti kati ya sppedmeters za polisi na za magari lakini hata 0.50% Hutozwa faini. hii sio sawa na ni uonevu tu.
Wenzetu hawaweki Vitochi bali kuna camera kuondoa ubishi na rushwa
Mara nyingi tuna tuna tungiwa sheria kama Taifa hili ni la outlaws....
 
Hivi kibao cha 50 kikiwekwa sehemu ya kanisa je ni lazima kukifuta siku ya jumatatu? Au vile vya mashuleni, ni lazima kuvifuata siku ya jumapili?
Kanisani huwa hawasali jumapili tu, waumini wapo free kwenda kusali kila siku kama maombi binafsi. Pia shuleni kuna masomo ya ziada ambayo yanaweza kufanyika siku yoyote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama lengo ni hilo, basi nchini hii pekee yanafanyika. La msingi tufuate tu sheria vibao viwekwe vya speed limit vionekane, na waache kujificha ili kupiga picha
Na pia vibao vya tahadhari kuwa unatakiwa kupunguza spidi mita kadhaa kabla ya kukifika kibao cha 50 viwekwe, hii ghafla unakiona kibao nalo ni tatizo la kiufundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hizo sheri ambazo zinahusu kosa moja, ni lazima sheria moja iwe na nguvu zaidi kuliko zote. Ile iliyo Na nguvu kuliko zote ndo inatakiwa kutumika. Haiwezekani faini zote hizo tatu ziwe katika kosa moja. Haileti maana
 
Tatizo ni mpiga picha kujificha mahali ambapo hakuna speed limit na akapiga picha na kuituma kwa askari aliyeko mbele. Hii ni kweli na inatokea sana. Shemeji yangu ni mpiga picha za barabarani na alinihakikishia hilo
Hii inaweza kuwa kweli eti eh!

"Do not compete with any one, do the best to become the best"
 
Waafrika bana yani issue ndogo imekuwa mjadala. Kwanini utokwe povu ilhali ukitembea bellow 80Km/hr hauna shida.
Ajali zikiwa nyingi lawama, ikiwekwa njia ya kuzuia lawama.

Sisi wenye haraka tupande ndege, na kama tunakoenda hakuna routes za ndege tukodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni uzushi mbweha nyie. Mimi baada ya kuona hapa, nimeenda kukanyaga mpaka 120 nikapigishwa faini ya 30,000 nikawauliza mbona wamechaji kosa moja tu, wakaniambie niachane na habari za vijiweni kwani hakuna faini ya aina hiyo duniani. Ukiharibu au kutishia kuharibu miundo mbinu ya barabara hapo ndiyo hukunyuka TANROADS faini
Asante
 
Barabara nyingi za ulaya hazina traffic police.. nyingi zina camera na toll stations. Toll station ni kama ile pale daraja la kigamboni.

Ukifanya kosa lets say Mlandizi, unakutana na toll station Chalinze. Huwezi kupita hapo mpaka ulipe faini.
Mh Ulaya niliokaa mimi ukizidisha speed ticket yako unaipata kwa posta baada ya muda usiozidi wiki mbili. Humo utaambiwa wapi,lini ulitenda hilo kosa na utapewa option ya kulipa fine au mahakamani ukiamua kupinga. At the same time uwapelekee details za insurance,license yako wakutwange points.
Toll unatumia kulipa ushuru wa barabara uliotumia ambayo ni ya kulipia.
 
Mbona suluhisho lake rahisi tu punguza spidi nenda mwendo unaoruhusiwa basi utaepuka hiyo faini ya nini mapovu?
 
Hao wanaopitisha hizo faini za laki mbili kwa kosa moja wanakuwa wapo usingizini au ni vipi! Ndio hivo walipitisha ile sheria ya Road licence act walivoona inawaumiza hata wao wakaamua kuifuta harakaharaka na serkali kuibadilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom