Hujanielewa mkuu, mi sisemei kuhusu maamuzi yao, kasoro ninayoiona ni namna wanavyoongea kama majaji.
Hebu soma comment ya mdau hapo No.14 ujue nilichomaanisha, amefafanua vizuri sana, namnukuu hapa ....U judge ni natural talent, ebu muone monalisa aki judge anavyojiachia yaani yupo free kuji express hisia zake kwa kiwango kinachotakiwa, hajazubaa mchangamfu na haboi.
Huyo roy anaweza kuwa hata na ma phd lakini u judge usi mfit, Yes the guy is boring somehow......
majaji wanajua sana... mleta uzi inaonyesha wewe huwa ndo unaanza kuwajudge
washiiriki hata kabla ya ma- judge kuwachambua...! thats y unawaona wanakosea..!!
Mkuu mito, unaposema Roy anakuboa na pia "ndio kabisa hajiwezi" kwa vipi yani? Naona sijakupata uzuri!
Huyo sarungi nimeshakutana nae kwenye pilika zangu. Kiukweli hana passion ya aina yoyote. Ni mkavu sana japo anaweza kuwa talentedJumapili moja moja nimekuwa nikifuatilia hii show ya TMT. Watangazaji wake (Joti na Lulu) kwa kweli nawakubali, wamejipanga vizuri. Majaji mmh, namkubali mmoja tu, Monalisa. Richie na yule sijui Sarungi wananiboa, hawana mvuta wa kuongea. Richie najua na bongo muvi mzoefu, tena wa siku nyingi lakini ameshindwa kuonyesha uzoefu wake ktk nafasi ya ujaji. Huyu mwenzake Sarungi (sina hakika sana na hili jina) ndo kabisaaa, hajiwezi!! Ila natamani kumjua zaidi, so kwa aliye na details zake tafadhali tumwagie, binafsi sijawahi kumuona bongo muvi.
Nionavyo mimi: Mwenye kipindi amefanya mabadiliko kwenye safu ya majaji, hawaondoe Richie na mwenzie halafu aweke vifaa vingine kama kina J.B, Wema and the like. Nahisi kipindi kingekuwa na mvuto wa kutosha na wadhamini wangejitokeza kwa wingi.
Huu ni mtizamo wangu jamani, msinishambulie!!!
Mkuu mito, unaposema Roy anakuboa na pia "ndio kabisa hajiwezi" kwa vipi yani? Naona sijakupata uzuri!
Anamaanisha hamuoni kwenye magazeti ya shigongo,so bado ajafuzu bongo muvi.