Uchezaji wa Movie na Uzuri wa mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchezaji wa Movie na Uzuri wa mtu

Discussion in 'Entertainment' started by Madenge, Jun 16, 2009.

 1. M

  Madenge Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nimekutana na hii harabari toka Global Publishers, baadhi ya wachezaji wa filamu wakiwaponda wasanii wenzao kuwa hawana mvuto wa kucheza filamu.
  Mimi nionavyo ni kuwa msanii inategemeana ni sehemu gani anatakiwa acheze na uwezo wake katika kuicheza sehemu hiyo. Hebu tujadilini hili naona hawa wasanii waliotoa maoni yao hapo chini wapo nje kidogo ya fani ya usanii...

  No mvuto ijumaa


  Katika mjadala huo, watayarishaji wengi wa filamu nchini walisema kuwa mamisi ni muhimu kutokana na mvuto wao, huku wakiwaponda wasanii wa kike ambao ni wakongwe katika kiwanda cha ‘muvi’ nchini kwamba wamechoka.

  Wakilumbana wakati wa kurekodi kipindi cha Bongo Movies cha Channel Five ambacho hurushwa hewani kila Jumatano saa 3:30 usiku, ‘maprodyuza’ wengi walisema kuwa wakongwe wa kike wengi wamejisahau na kupoteza mvuto.

  Watayarishaji waliohojiwa ni Steven Charles Kanumba, Vincent Kigosi ‘Ray’, Single Mtambalike ‘Richie’, Jacob Steven ‘JB’, George Otieno ‘Tyson’, Musa Isa ‘Cloud’ na wengineo.

  Aidha, wasanii wakongwe Riyama Ali, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Yvonne Cherry ‘Monalisa’, Blandina Chagula ‘Johari’ walihojiwa kwenye kipindi hicho na kupinga madai kwamba hawana mvuto na kueleza kuwa mamisi si waigizaji bali ni wauza sura.

  Akihojiwa na mtangazaji Joyce Kiria wa kipindi hicho ambacho kitarushwa Jumatano hii, Kanumba alisema kuwa mamisi wanaongeza mvuto kwenye filamu kwa sababu waigizaji wakongwe wanajiachia na kupoteza mvuto wa awali.

  Kanumba aliwataka wasanii wakongwe kulinda mvuto wao wa asili ili waendelee kupata soko la kucheza filamu, vinginevyo mamisi wataendelea kutawala fani kwa sababu muonekano wao unauza.

  “Mamisi wanajilinda, wanajitunza lakini wasanii ambao ni wakongwe ‘wananenepeana’ na wengine wamechoka,” alisema Kanumba na kuzidi kupigia msumari kwamba wakongwe wengi wa kike nchini hawauzi filamu.
  “Katika biashara ya filamu sasa hivi, mvuto ndiyo kila kitu kwahiyo urembo unaangaliwa kwanza halafu ndiyo tunageukia vipaji,” alisisitiza Kanumba a.k.a The Great.

  Kwa upande wake Ray, alisema kuwa ni ngumu kuuza filamu kwa kuwatumia wanawake wasiokuwa na mvuto, hivyo mamisi wana haki zote za kutawala ‘game’ kwa kipindi hiki.

  Ray alikiri kwamba hivi sasa tabaka la wasanii ambao ni ‘freshi’ kutoka kwenye mashindano ya urembo wamekuwa ni wazuri kibiashara kuliko wakongwe ambao chati yao inashuka kila kukicha.

  Miss Tanzania 2006-07, Wema Sepetu, Miss Tanzania namba tano 2006-07, Irene Uwoya, Miss Mwanza 2006-07, Aunt Ezekiel ni baadhi ya waigizaji waliotokea kwenye fani ya urembo wakati Johari, Thea, Mona na wengine ni wakongwe katika sanaa za maigizo nchini.

  “Kila mtu anaweza kuigiza, wanawake wazuri waje kwangu nitawapa nafasi, nitawapa maelekezo na wataweza. Biashara ya filamu tunajali zaidi mvuto wa mtu,” alisema Ray.

  Prodyuza mwingine, JB alieleza kuwa mwanamke mzuri ni pambo, kwahiyo filamu itakuwa bora zaidi endapo itapambwa na wasanii wa kike wenye mvuto ndiyo maana soko la mamisi limekuwa kubwa kwenye kiwanda cha muvi nchini.
  Tyson alisema kuwa kitu pekee ambacho anakiangalia kabla ya kuandaa muvi yoyote ni ubora wa wahusika, kwahiyo huzingatia zaidi wanawake wazuri na wenye majina makubwa.

  Aliongeza kuwa mwanamke mwenye nafasi ya ‘kuuza sura’ kwenye muvi zake ni lazima awe mrembo, hivyo akawataka wale ambao mvuto wao ni wa wasiwasi, wasubiri mpaka pale kutakapokuwa na hitaji la mtu asiyevutia katika filamu yake.

  Cloud pia alitoa mawazo ambayo hayakutofautina na ya akina Ray, Kanumba na Tyson, lakini Richie kwa upande wake alieleza kuwa kipaji ni muhimu kuliko urembo, kwahiyo kwenye muvi zake huangalia anayeweza kuigiza.
  Wakipangua hoja ya kutokuwa na mvuto, Johari na kundi lake walisema kuwa wao kama wasanii wakongwe bado wanavutia na kazi wanaiweza ndiyo maana bado wapo juu.

  Wasanii hao pia walihoji aina ya mvuto ambao unatakiwa na maprodyuza kwa sababu hata wao si haba na kuponda wimbi la mamisi walioingia kwenye filamu kwamba wengi wao wanauza sura tu lakini hawawezi kazi.

  “Mbona sisi mvuto tunao, tena na kazi tunaiweza labda tuambiwe huo mvuto unaotakiwa ni wa namna gani, sisi tupo juu, hao mamisi wanakuja tu kuuza sura sura” alisema Monalisa wakati akiwasilisha utetezi wake kwa Joyce.
  Katika kujieleza, mtazamo wa Monalisa ulishabihiana na ule wa Thea, Riyama na Johari ambao ndiyo magwiji pekee wa kike waliohojiwa katika kipindi hicho.

  Kipindi cha Bongo Movies mbali na kurushwa hewani na Channel Five kila Jumatano saa 3:30 usiku, pia hurudiwa Alhamisi saa 6:30 mchana, pia Jumapili saa 12:00 jioni.
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mmh kwa heri, wenye "mada" endeleeni kujadili, thought it's something health!!
   
Loading...