anzisha chakoJumapili moja moja nimekuwa nikifuatilia hii show ya TMT. Watangazaji wake (Joti na Lulu) kwa kweli nawakubali, wamejipanga vizuri. Majaji mmh, namkubali mmoja tu, Monalisa. Richie na yule sijui Sarungi wananiboa, hawana mvuta wa kuongea. Richie najua na bongo muvi mzoefu, tena wa siku nyingi lakini ameshindwa kuonyesha uzoefu wake ktk nafasi ya ujaji. Huyu mwenzake Sarungi (sina hakika sana na hili jina) ndo kabisaaa, hajiwezi!! Ila natamani kumjua zaidi, so kwa aliye na details zake tafadhali tumwagie, binafsi sijawahi kumuona bongo muvi.
Nionavyo mimi: Mwenye kipindi amefanya mabadiliko kwenye safu ya majaji, hawaondoe Richie na mwenzie halafu aweke vifaa vingine kama kina J.B, Wema and the like. Nahisi kipindi kingekuwa na mvuto wa kutosha na wadhamini wangejitokeza kwa wingi.
Huu ni mtizamo wangu jamani, msinishambulie!!!
Wema nae awe judge kwa lipi hasa wakati yeye mwenyewe hata kuigiza hawezi
Huyo unayomsema hawezi ujaji(roy sarungi) amepata tuzo 45 za kimataifa ni msomi ana degree ya sheria ameanzisha vipindi naijeria na vinapendwa sana huko kwa wapopo ni moja ya wataaalamu ktk tasnia ya bongo movie.
sema wewe nikisema mimi nitaambiwa mchawi, kuigiza kwenye huyo mama ubaya kumemshinda haya uo u judge ata judge nini? we mwambie kucheza kigodor mtaelewana
U judge ni natural talent, ebu muone monalisa aki judge anavyojiachia yaani yupo free kuji express hisia zake kwa kiwango kinachotakiwa, hajazubaa mchangamfu na haboi.
Huyo roy anaweza kuwa hata na ma phd lakini u judge usi mfit, Yes the guy is boring somehow, japokuwa namkubali sana nadhan ni mmoja wa ma boss wa tmt, inshort kampuni yao imejipanga vibaya, kwanza inaendeshwa na watu wasomi na wanaojielewa, kingine wapo financially strong na wako serious na wanachokifanya, nadhan wataleta mapinduzi kweny mambo ya film
majaji wanajua sana... mleta uzi inaonyesha wewe huwa ndo unaanza kuwajudge
washiiriki hata kabla ya ma- judge kuwachambua...! thats y unawaona wanakosea..!!
Kama we huwakubali kuna wenzio wanawakubali ambao wanafatilia daily.MTU mwenyewe ushasema huwa unafatilia j2 moja moja.hata hapo we ulipo kuna wanaokukubali na wanaokuchukia uwepo wako mkuu.km unaona we huwapendi basi usitazame hicho kipindi.acha wenzio tusonge mpk tujue nani anakuwa mshindi