TLS: Sisi tunaendelea na maandalizi ya Uchaguzi, ya Mwakyembe hayatuhusu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,886
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimesema kuwa kitaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wake licha ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kutishia kukifuta kwa madai ya kujihusisha na mlengo wa kisiasa.

Mvutano huo baina ya TLS na Serikali umekuja zikiwa zimebaki siku kumi kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi huo ambao kwa mara ya kwanza umekuwa na msisimko na vuta ni kuvute kati yake na Serikali.

Dkt. Mwakyembe alisema Serikali haitakubali kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa, bali itafuta sheria iliyoianzisha sura ya 307.

Aidha, Rais wa TLS, John Seka amesema kuwa chama hicho hakijajiingiza kwenye siasa na wataendelea na maandalizi ya uchaguzi wao kama kawaida ambao unatarajiwa kufanyika machi 18, mwaka huu.

“Alichokisema Mwakyembe ni kauli ya Serikali lakini sisi tutaendela na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida na kama Ilivyopangwa,”amesema Seka.

Hata hivyo, Seka amesema kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wa kuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati.
 
Wakomae hivo hivo, wasikubali kuburuzwa na kufanya matakwa ya serikali

Uchaguzi usipoingiliwa na akapatikana mtu sahihi, itakuwa a step in the right direction kuikomboa hii nchi inayokwenda shimoni
 
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimesema kuwa kitaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wake licha ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kutishia kukifuta kwa madai ya kujihusisha na mlengo wa kisiasa.

Mvutano huo baina ya TLS na Serikali umekuja zikiwa zimebaki siku kumi kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi huo ambao kwa mara ya kwanza umekuwa na msisimko na vuta ni kuvute kati yake na Serikali.

Dkt. Mwakyembe alisema Serikali haitakubali kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa, bali itafuta sheria iliyoianzisha sura ya 307.

Aidha, Rais wa TLS, John Seka amesema kuwa chama hicho hakijajiingiza kwenye siasa na wataendelea na maandalizi ya uchaguzi wao kama kawaida ambao unatarajiwa kufanyika machi 18, mwaka huu.

“Alichokisema Mwakyembe ni kauli ya Serikali lakini sisi tutaendela na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida na kama Ilivyopangwa,”amesema Seka.

Hata hivyo, Seka amesema kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wa kuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati.
Mwakyembe achunguzwe ni kwa njia gani alipata huo udokta
 
Kauli za mhe. Mwakye zinaonyesha anahofu na kitu fulani.. au mtu fulani. Kwanin anataka kuingilia mamlaka ya TLS
 
Kuna mtu aliyewahi kumsikia Mwakyembe akitetea CHOCHOTE mahakamani
The guy is all hot air,nothing practical
 
Lisu anakwenda kumsaidia Rais kunyoosha tls kama anavonyoosha yeye anavonyoosha nchi,sasa mwakyembe hataki,kwanini hashtakiwi kwa kupinga wazi wazi kusudio la Rais?
 
Mwakyembe sijui alipataje udokta inabidi afanyiwe uchungunzi awezi kua anongea pumba hivyo alafu anajiita msomi
 
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimesema kuwa kitaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wake licha ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kutishia kukifuta kwa madai ya kujihusisha na mlengo wa kisiasa.

Mvutano huo baina ya TLS na Serikali umekuja zikiwa zimebaki siku kumi kabla ya chama hicho kufanya uchaguzi huo ambao kwa mara ya kwanza umekuwa na msisimko na vuta ni kuvute kati yake na Serikali.

Dkt. Mwakyembe alisema Serikali haitakubali kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa, bali itafuta sheria iliyoianzisha sura ya 307.

Aidha, Rais wa TLS, John Seka amesema kuwa chama hicho hakijajiingiza kwenye siasa na wataendelea na maandalizi ya uchaguzi wao kama kawaida ambao unatarajiwa kufanyika machi 18, mwaka huu.

“Alichokisema Mwakyembe ni kauli ya Serikali lakini sisi tutaendela na maandalizi ya uchaguzi kama kawaida na kama Ilivyopangwa,”amesema Seka.

Hata hivyo, Seka amesema kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wa kuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati.
SAWA: so what?
 
Back
Top Bottom