Tlp na udp si vyama vya upinzani?

Tlp na udp si vyama vya upinzani?

Diplomatician

Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
21
Reaction score
1
Bila shaka Suala kubwa na la Msingi nchini kwetu ni kuhusu Suala la Mchakato wa Katiba Mpya.
Sisi sote ni Mashahidi kua Vyama vya Upinzani Pamoja na Wadau wengine Wenye Mapenzi Mema Na nchi Yetu wamekua Mstari wa Mbele Kutetea Mchakato wa Katiba Mpya kua Mchakato Shirikishi kwa Wananchi Wenyewe na Si Kuhodhiwa Na Chama Tawala kama Ilivyodhihirishwa Wakati wa Mjadala Wa Mswada wa Sheria inayoelekeza Jinsi gani Bunge la Katiba lipatikane na Namna nzima Ya Majadiliano Hayo.

Cha kushangaza Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustine Mrema alibaki Peke yake Bungeni kama Mbunge wa Chama cha Upinzani akishirikiana na wabunge wa Chama Tawala kupitisha Ule Mswada wakati wa Mjadala amabapo Wabunge wenzake wa Vyama vingine vya Upinzani walitoka Nje kususia Mjadala wa Mswada wenye utata.

Kama hiyo haitoshi Siku ya Juzi,21 Sept Pale Jangwani wakati Vyama vya Siasa Vya Upinzani Na Wadau Wengine Wakitoa yao ya Moyoni Kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya Sikusikia Mwakilishi hata Mmoja akitajwa Kukiwakilisha Chama Cha TLP Hali kadhalika Kwa Upande Wa UDP hali ni ile ile,Nakumbuka kua Kama sikosei wakati wa Mjadala wa Ule mswada katika Bunge lililopita Mh. John Momose Cheyo Mb. Pekee na Mwenyekiti kutoka UDP Hakuwepo Bungeni(Kama nimekosea naomba Kusahihishwa)Lakini kutokuwepo kwake hakuzuii Chama chake kutoungana na Vyama Vingine vya Upinzani kutetea Mchakato wa Katiba Uwe Shirikishi kama Wadau wengine wenye Mapenzi Mema Wanavyotetea.
Je,Ukimya wao huo,wanatuaminisha kua Sasa UDP na TLP Si vyama vya Upinzani?
 
Tatizo ni wenyeviti wao. Cheyo anaumwa yuko India ingawa ni wale wale. Mrema ni . . . . . . . !
 
Hawa watu hawajawahi kuwa upinzani. Shida yao ni matumbo...Cheyo naona mambo kiuchumi hayamwendei vema na ndiyo maana hata sera yake ya utajirisho wa kuwajaza watu mahela mifukoni imekufa kwa hiyo sasa anasubiri mpiga gitaa aweze kumchezea ngoma yake ili apate kula. Mrema, kila mmoja anaona jinsi alivyorusi bungeni safari hii. sidhani kama kweli huyu jamaa alishinda. Yeye huyu ni mwanaccm mtiifu kwa chama chake. Ameona siku zimeenda na amepata maradhi mengi mwilini yanayomsumbua...akifikiri sana anaona hakuna mtu wa kumbeba asipokuwa na ccm iwapo mambo yataharibika, hivyo ameamua kumtumikia kafiri...ili apate mtaji wake. Kuna upinzani hapo?
 
Back
Top Bottom